Katibu wa Itikadi,siasa na uenezi Humphrey Polepole
amewaongoza mamia ya wananchi viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM)
katika hafla ya kumpokea Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne Edward
Lowasa Wilayani monduli Mkoani Arusha.
Katika hafla hiyo Polepole amesema Chama Cha mapinduzi ni
chama kinacho zitangatia sheria na taratibu za chama katika mambo
mbalimbali kwa maslahi ya wananchi na ndani na nje ya CCM.
"Nilazima kufata taratibu zote za kisheria kwa mujibu wa
katiba ya CCM kwa yeyote atakae jiunga na chama Cha mapinduzi ili kuweza
kuendeleza Maendeleo ya nchi vinginevyo hatuta mpokea Wala kumruhusu
mtu kujiunga na CCM"alisema Polepole.
Muda mchache baadae Mara baada ya kila kiapo Pamoja na
wanachama wapya walio jiunga na chama tawala nchini Tanzania (CCM)
Waziri mkuu mstaafu Edwad Lowasa akatumia halfa hiyo kuwataka watanzania
kudumisha amani na ushirikiano chanya kwa maslahi ya Taifa ili kuendana
na Kasi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Amesema ameamua kuridi CCM Kutokana na kazi, juhudi kubwa
na uzalendo unaofanywa na Rais Magufuli hivyo ni wakati muafaka kuunga
mkono juhudi hizo ili kusukuma gurudumu la Maendeleo mbele kwa
ushirikiano na serikali ya awamu ya tano.
"Nimeamua kurudi nyumbani Sina sababu zaudi ya kusema Kuwa
nimerudi nyumbani, nashukuru Sana (CHADEMA) nimejifunza mengi sana"
alisema Lowasa.
Msumba news imepata Fursa ya kuzungumza na baadhi ya wakazi
wa Wilaya ya Monduli akiwemo mwenyekiti wa viongozi wa kimila maarufu
laigwanani Bw:Kisongo ole meijo na Ole Kalanga kitutu ambapo wamesema
ujio wa Lowasa ni faraja na furaha kwa wakazi wa monduli kwa ujumla ili
kuchochea Maendeleo katika Wilaya hiyo.
Ole meijo amesema kwa muda mrefu kumekucha na matabaka
katika jamii ya wafugaji suala ambalo limekuwa chanzo Cha baadhi ya
migogoro na kuduma Maendeleo hivyo wanategemea mazuri kwa ushirikiano na
serikali ya watanzania.
"Lowasa atatuunganisha vyema na Rais Magufuli kwa ajili ya
utatuzi wa kero ya maji kwa muda mrefu tunaamini Mambo yataenda sawa".
Lowasa amepokelewa na viongozi wa chama hivi karibuni Mara
baada ya kukihama chama Cha CCM nyakati za Uchaguzi mkuu 2015 na
kuelekea (CHADEMA) huku akiwa ameongoza Jimbo la Monduli kwa zaudi ya
Miaka 24 kwa tiketi ya chama Cha mapinduzi CCM.
Post A Comment: