Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sebaya amesema marehemu Charles Ole Ngereza ndiye aliempatanisha na waandishi wa Habari aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti.
Akitoa salamu za mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti Mkuu wa wilaya ya Hai alisema "wakati waandishi walipopishana na waandisi wa habari akiwa mkuu wa wilaya ya Arumeru,mimi nilimtafuta Charles Ngereza nikiwa Diwani huko Arumeru nikamwambia kaka Mnyeti anagombana na waandishi wa Habari na wewe ni kaka yao,tafadhali tusaidie ugomvi huu uishe,Tukamchukua Ngereza akamuita Gwandu,Pamela na Mustafa na tukaenda kuzungumza na waandishi wa Habari.
Amesema Kati ya Maneno ambayo Ngereza aliwaambia Press Club ya Arusha [APC],"Maisha haya siyo ya kudumu,kwa hiyo ugomvi utawasidia nini?,Tukaombana msamaha yakaisha ukafunguliwa ukurasa mpya,kwa hiyo Ngereza ni mpatanishi,na heri hao wapatanishi maana hao ni wana wa Mungu,leo amepumzika kwenye miguu salama ya Yesu."alimaliza hivyo mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sebaya akitoa salamu za Rc Mnyeti.
Mwaka 2016 Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha kwa umoja wao waligoma kwenda ziara ya Waziri wa Ardhi William wakinishikiza kuachiwa huru kwa mwenzao wa ITV Halfan Liundi ambaye aliwekwa ndani kwa amri ya Dc Mnyeti akimtuhumu kuripoti taarifa ya maji ambayo hakuipenda na kuwa ilikuwa ni habari ya uchochezi.
Post A Comment: