Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub akizungumza wakati wa warsha hiyo |
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo wakati wa warsha hiyo |
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo |
Sehemu ya wajumbe wa warsha hiyo wakifuatilia |
KUKOSEKANA
elimu kwa wajumbe wengi waliopo kwenye mabaraza ya ardhi na nyumba ngazi ya
kata kumeelezwa kuchangia kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa waledi mkubwa
na kusababisha migogoro kwa wananchi na manung’uniko.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Tanga Doris
Wilson wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa ngazi mbalimbali ikiwemo
mabaraza,wenyeviti na wajumbe juu ya ujuaji wa sheria na kufata taratibu na
kutoa maamuzi sahihi ili kuweza kutatua migogoro ulioandaliwa na Chama cha
Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) na kufanyika mjini hapa.
Alisema elimu
hiyo itakuwa chachu kwa wajumbe hao kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku
kwenye mabaraza hayo lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha wanatenda haki kwa
wananchi ambao wanakabiliwa na migogoro mbalimbali kwenye maeneo yao.
“Changamoto kubwa
ya mabaraza ya Kata ni elimu wajumbe wengi hawajapata elimu kuhusu mabaraza
hayo, muundo, namna ya utendaji, akidi katika kuendesha na utaratibu wa
kuendesha mashauri hivyo tunaamini kupitia elimu hii inaweza kuleta mabadiliko
makubwa kwenye utekelezaji wa shughuli zenu “Alisema Mwenyekiti huyo.
“Lakini pia
tunaishukuru Tawla kwani wanapotoa mafunzo ya namna hii wanawapa wajumbe uelewa
kuhusu namna ya kuendesha mashauri hayo,kwa kufanya hivyo haki kwa wananchi
inaweza kutendeka na kuondoa manung’uniko “Alisema
Aidha alisema
mikakati waliokuwa nayo hivi sasa ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa mabaraza ya
ngazi ya kata ili waweze kufanya kazi zao kwa waledi mkubwa katika kutoa haki
pindi wanapopelekewa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Awali
akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake
Mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub alisema lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu
kwa ngazi mbalimbali kwa viongozi wa mabaraza,wenyeviti na wajumbe ili waweze
kujua sheria na kufuata taratibu na kutoa maamuzi sahihi wakati wakitatua
migogoro.
Mratibu huyo
alisema warsha hiyo imehusisha wajumbe, makatibu na wenyeviti wa mabaraza ya
ardhi kutoka kwenye kata mbili za Magila na Kilulu kwalengo la kuwajengea uwezo
wa kufahamu sheria za ardhi na kuto maamuzi sahihi kwa wananchi.
Hata hivyo
alisema watajaribu kuangalia jinsi gani ya kuweza kushirikiana kwa pamoja
kupunguza changamoto hizo yakiwemo mashauri mengi yaliwepo kwenye baraza hilo
hali itakayowezesha kuondosha migogoro kwa wananchi.
Post A Comment: