Na Karim Juma - Mboga -chalinze
RAIS Mstafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekagua maendeleo ya shule ya sekeondari Mboga na kujiridhisha kwa utendaji wa bodi ya shule hiyo na bodi ya shule hiyo kuhitajika kuachia madaraka kufuatia na waraka uliotolewa na Wizara ya elimu kwa shule za sekondari .
Dkt. Kikwete amesema kwamba uchagauzi wa bodi mpya ufuate maelekezo kama yaliyotolewa kwenye waraka huo na sio kumchagua mtu kwa umarufu alionao, Hata hivyo kikwete aliomba wanafunzi na walimu watunze shule kwa kuwa ni ya kisasa sana na bado itaendelea kuwekezwa kwa kupata elimu ya kidato cha tano na cha sita.
Amesema kuwa kwa wakati huu wakiendelea na utengenezaji wa majiko ya kupikia na wamepanga kujenga bwalo la chakula kwa wanafunzi pamoja na sehemu ya kuhifadhia chakula.
Pia Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amesema ameridhishwa na uwajibikaji, utendaji kazi kwa kuonesha kauli mbiu ya hapa kazi inatekelezwa hasa kwa bodi ya shule kujinyima posho ili shule iweze kuwa salama na kuweza kukamilika pamoja na kupata watendaji wa kufundisha vijana kwa ufasaha.
Ridhiwani amesema ni wakati sasa kwa Halmashauri ya Chalinze kutumia pesa za ndani kuweza kuwapa posho walimu wa kujitolea kwa kuwa kuna uhaba wa walimu wasayansi na kwa hali ya sasa ya dunia inanyoendeleha lazima kupate wataalamu wa mambo ya teknolojia.
Post A Comment: