Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo
cha Mtangazaji wa Clouds FM, Efraim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani
kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia,
Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimfariji Hilda Samson Kibonde ambaye ni mama
mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde wakati alipokwenda
nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam, kutoa pole
kwa familia, Machi 8, 2019. Katikati ni baba mzazi wa marehemu,
Samson Job Kibonde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Samson Job Kibonde ambaye ni baba mzazi wa Mtangazaji wa Clouds FM, Ephrim Kibonde wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu, Mbezi Beach jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia, Machi 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha aliyekuwa Mtangazaji Muandamizi
wa kituo cha redio cha Clouds, Ephraim Kibonde ni pengo kubwa kwa Taifa,
Clouds Media Group na tasnia ya habari kwa ujumla.
Ameyasema
hayo leo (Ijumaa, Machi 8, 2019) alipokwenda kuhani msiba wa Mtangazaji
Muandamizi kituo cha redio Clouds, Kibonde kwa niaba ya Rais Dkt. John
Magufuli, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mbezi Beach Dar es Salaam.Kibonde alifariki dunia jana alfajiri Machi 7, 2019 jijini Mwanza.
“Msiba
huu umetushtua sana na ni tukio ambalo hatukulitarajia ila ni mapenzi
ya Mwenyezi Mungu. Hivi karibuni sote tulimshuhudia akiongoza ratiba ya
kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media
Group, Ruge Mutahaba na alienda hadi Kagera kumzika.”
Waziri
Mkuu amesema marehemuKibonde enzi za uhai wake ameshirikiana vizuri na
Serikali katika shughuli mbalimbali, hivyo amewaomba wananchi waendelee
kushikamana na kuifariji familia. “Tumuombee marehemu apumzike kwa
amani.
Kadhalika,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na
wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi
hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, MACHI 8, 2019.
Post A Comment: