Shaka Hamdu Shaka Katibu CCM Morogoro kushoto akitazama bidhaa za wanawake wajasiriamali
Taifa lolote lisilothamini mchango wa wanawake ni butu,
dhana ya usawa wa kijinsia ni kichocheo cha ushiriki na ushirikishwaji
katika maendeleo endelevu ya kila Taifa linalothimini na kujali mchango
wa kina mama.
Baba wa Familia ya watanzania Rais John Pombe Joseph
Magufuli alisema asubuhi ya leo 8 Machi 2019 kuwa serikali
anayoiyongoza inathamini kazi nzuri inayofanywa na akina mama, amewataka
muendelee kutembea kifua mbele.
Nasi wasaidizi wake katika Chama cha Mapinduzi tunamuunga
mkono kwenye hilo ninawahakikishia tutawapa kila aina ushirikiano, msaada na tutawashika mkono wanawake wa Morogoro na watanzania kwa
ujumla ili muweze kufikia ndoto zenu maana hata ilani ya CCM
2015-2020 imetuelekeza kusimamia na kuendeleza harakati za maendeleo ya
wanawake kiuchumi, kijamii na kiasiaza nchini.
Shaka Hamdu Shaka
Katibu CCM Morogoro
Katibu CCM Morogoro
Post A Comment: