Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias
Kwandikwa, akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu
kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Mizani kinachojengwa Dakawa
Mkoani Morogoro, wakati kamati hiyo ilipokagua mzani huo. Wa nne kushoto
ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Suleiman Kakoso.
Mafundi wa Kampuni ya Group Six
International wakiendelea na ufungaji wa Kamera katika mzani mpya
unaojengwa eneo la Dakawa mkoani Morogoro.
Muonekano wa jengo la mzani mpya unaojengwa Dakawa Mkoani Morogoro. Mradi huo umekamilika kwa asilimia 98.
Mhandisi Mshauri Kasmir Mustapha
(kulia), akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu
kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Mizani kinachojengwa Dakawa
Mkoani Morogoro, wakati kamati hiyo ilipokagua mzani huo.
………………………
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu imeishauri Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kujenga nyumba za watumishi kwenye mzani
mpya unaojengwa Dakawa Mkoani Morogoro ili kuwapunguzia adha wafanyakazi
watakaokuwa wakifanya kazi kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya kukagua
mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Sulemani Kakoso
ameipongeza Wizara na kuhakikisha kuwa pamoja na kujengewa nyumba hizo,
pia Wizara iwasimamie watumishi wa mzani vizuri ili kuepuka vitendo vya
rushwa.
“Serikali imetumia fedha nyingi
kujenga mzani huu, nawapongeza sana lakini sasa ni muhimu watumishi wa
mzani huu wakasimamiwa vyema ili kuepuka vitendo vya rushwa
vinavyofanywa na watumishi wasio waaminifu” amesema Mwenyekiti. Kakoso.
Mwenyekiti Kakoso, ametoa wito kwa
wafanyabiashara wote nchini kuhakikisha wanazingatia sheria za mizani
kwa kupakia mizigo isiyozidi kiwango ili kulinda miundombinu ya barabara
nchini.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa
Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Serikali
imejipanga kuhakikisha changamoto zote zilizowasilishwa zinatatuliwa
mapema ili kuongeza ufanisi.
Naibu Waziri huyo ameieleza kamati
hiyo kuwa ujenzi wa mzani huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi
Machi mwaka huu kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 14.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Usalama
na Mazingira kutoka Sekta ya Ujenzi Mhandisi Julius Chambo, amesema
ujenzi wa mzani huu unatokana na mzani wa Kihonda kuzidiwa na msongamano
wa magari kwa kuwa ni wa upande mmoja.
Ameeleza kuwa ukamilikaji wa mzani
huu utasaidia kuokoa muda kwa wasafirishaji na kuondosha msongamano
uiopo sasa katika mzani wa Kihonda kwani mzania huu utapima tu yale
magari yanayoonekana yamezidi uzito tu.
Post A Comment: