Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing (WHC), Dk Fred Msemwa akifafanua jambo wakati akitoa maelezo kwa  Kamati ya Bunge ya  Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati ilipotembelea na kukagua miradi ya WHC iliyopo Kigamboni Gezaulole na Bunju jijini Dar es salaam.
Kamati ya Bunge ya  Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakikagua Mradi wa WHC iliyopo Kigamboni Gezaulole jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya nyumba za WHC zilizopo Kigamboni Gezaulole jijini Dar es Salaam.
 Miradi ya WHC iliyopo Bunju B jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing (WHC), Dk Fred Msemwaakitoa maelezo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuiongoza Kamati ya Bunge ya  Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati ilipotembelea na kukagua miradi ya shirika hilo iliyopo Kigamboni Gezaulole na Bunju jijini Dar es salaam.




Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeitaka Taasisi ya Watumishi Housing (WHC) kuendelea kuwa wabunifu wa kijenga nyumba na kuuza gharama nafuu na kutoa muda wa miaka 25 kwa mkopaji ili aweze kulipa deni lake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati kamati hiyo ikifanya ziara ya kukagua miradi ya WHC iliyopo Gezaulole Kigamboni pamoja na Bunju B, Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge na Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Negy Kaboyoka, amesema kuwa wamelizika na utendaji wa WHC katika utekelezaji wa miradi yao.

Mhe. Kaboyoka amesema  kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua nyumba za WHC ili kuona kama fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii zinatumika kama zilivyokusudiwa.
"Tunakagua fedha za wananchi ambazo WHC wamekopeshwa na mifuko ya hifadhi ya jamii zinatumika kama zilivyokusudiwa, nyumba zina ubora na zinapangishika" amesema Mhe. Kaboyoka.

Mhe. Kaboyoka alifafanua kuwa tunafanya ziara hii ili kuhakikisha fedha za wananchi zisitumike tofauti na kusababisha mifuko ya hifadhi ya jamii kufilisika.

Hata hivyo amesema kuwa licha ya ubora wa nyumba za WHC, lakini kuna vitu vinapaswa kufanyiwa kazi ikiwemo kurekebisha miundombinu ya barabara, huduma za kijamii, zahanati pamoja na shule ya awali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa WHC Dkt. Fred Msemwa, amesema  kuwa WHC inaendelea a njia mbalimbali za kibunifu ili kuhakikisha kila mtu anamiliki  nyumba yake kwa gharama nafuu.

Dkt. Msemwa amesema kuwa katika mradi Gezaulole Kigamboni umekamilika kwa asilimia 95 na sasa  wapo katika hatua ya mwisho ujenzi wa miundombinu ya barabara.

"Mradi wa bungu B umekabilika kwa asilimia 98 na tayari baadhi ya familia 20 wameaza kuishi" amesema Dkt. Msemwa.

Amesema kuwa kwa sasa wamefungua fursa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kuweza kukopa nyumba WHC katika miradi yao iliyopo katika mikoa I9 hapa nchini.

Dkt. Msemwa amefafanua kuwa kwa sasa kuna utaratibu wa mnunuzi mpangaji ambaye ni mtu yoyote anayepewa mkopo wa nyumba kutoka WHC na kuanza kuishi, huku akiendelea  kulipa deni lake kwa awamu.

Amesema kuwa kufanya hivyo inampa fursa mtanzania mwenye kipato cha chini   kumiliki nyumba kuliko kuendelea kuwa mapangaji bila kuwa na faida.

Amesema  kuwa lengo la WHC ni kuhakikisha kila mtu anakuwa na makazi bora, huku akibainisha sasa wapo katika kutekeleza mpango wa kujenga nyumba 500 katika Mkoa wa Dodoma.

Ameeleza kuwa watanzania wanapaswa kuendelea kujitokea WHC kwa ajili ya kununua au kukopa nyumba kwa bei nafuu kwa ajili ya kupata nyumba bora za kisasa.
WHC ni taasisi ya umma ambayo ilianzishwa mwaka 20I3 inayojihusisha na ujenzi wa nyumba za bei nafuu pamoja na usimamizi katika miliki.

WHC inafanya kazi kwa ushirikiano na mashirika yote ya Pensheni ikiwemo Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa Serikali (GEPF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi wa Jamii (NSSF), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PPF).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: