Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars itacheza game ya mwisho ya marudiano ya michuano ya kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 dhidi ya timu ya taifa ya Uganda siku ya Jumapili ya March 24 2019, mchezo huo ukiwa ni muhimu kwa Tanzania kupata ushindi ili wafuzu.
Kuelekea mchezo huo ambao ni muhimu kwa Tanzania, Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga ameamua kutoa tiketi 100 kwa watanzania kwenda uwanjani kuisapoti Tanzania wakati Taifa Stars ikiwa inacheza mchezo huo muhimu kwa Taifa.
Hizo tiketi 100 zishatoka, nitazitoa kabisa. Naomba shabiki atakaepiga simu ili kujishindia tiketi aanze kwa kusema#NaiombeaUshindiTaifaStars niliongea na wakuu wa vipindi Shaffih na Sebastian na tumekubali kwa moyo wa kizalendo kama vijana wa kitanzania ambao tumepata nafasi ya kuwa na platform ya kusaidia maendeleo na mambo mengine nguvu zetu zote tunazielekeza kuhamasisha watanzania kwenda mbele kwenye mambo mengi sio mpira peke yake”>>>Joseph Kusaga
Utaratibu maalum utatangazwa kwa ajili ya mashabiki kujishindia tiketi hizo 100 alizozitangaza Joseph Kusaga kuzitoa bure kwa mashabiki, kupitia Power Breakfast ya Clouds FM, Tanzania inahitaji ushindi pasipo kujali matokeo ya game ya Cape Verde dhidi ya Lesotho ambayo kama ikiisha kwa sare na Tanzania na Uganda wakamaliza kwa sare Taifa Stars itafuzu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: