Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema kuwa mpango wake wa kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 katika jimbo la Hai lililopo mkoani Kilimanjaro linaloongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe suala hilo linahitaji neema za Mungu.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na EATV, amesema kuwa ni kweli kumekuwa na maneno ya watu wengi wanaodai kuwa anaonekana mara kwa mara akifanya harambee kwenye jimbo la Hai.

“Hakuna binadamu anayeishi bila matamanio, mimi siwezi kusema matamanio yangu ni nini lakini Mungu akisema uwe Mbunge utakuwa lakini akisema usiwe Mbunge hata ufanye harambee 500 hutakuwa Mbunge, niwaambie watanzania masuala ya Ubunge yanahitaji kumtazama Mungu,”amesema Muro

Aidha, amesema kuwa watu wanaosema kuwa yeye anataka kugombea ubunge mwaka 2020 kwenye jimbo hilo wanamatamanio yao kwamba yeye awe mbunge wao, hivyo amewataka wafikishe salamu kwa Mbowe.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: