NA HERI SHAABAN

MANISPAA ya Ilala imesema itawachukulia hatua za kisheria Wafanyabuashara wa Manispaa hiyo watakaokaidi kulipia mapato ya halmashauri hiyo.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo na Ofisa Mapato wa Manispaa Ilala James Bangu wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari Arnatogluo Wilaya ya Ilala.

James alisema kuanzia Aprili Mosi halmashauri hiyo itaanzisha oparesheni kabambe kuwasaka wafanyabiashara wake watakaoshindwa kulipa Kwa wakati leseni zao pamoja na huduma ya kodi service levy.

Oparesheni hiyo kwa wafanyabiashara wasiolipa leseni na huduma ya kodi itaanza rasmi Aprili Mosi Mwaka huu na Wafanyabiashara watakaokamatwa watafikishwa katika vyombo vya sheria.

"tunatarajia kukusanya kodi ya mapato shilingi bilioni 56 mwaka wa fedha 2019/2020 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo kodi ya huduma service levy "alisema James

James alisema katika makusanyo ya fedha hizo bilioni 56 shilingi bilioni 15 zinatoka katika hushuru wa huduma.

Alisema manispaa ya Ilala imetoa siku tano kuwataka wafanyabiashara wote kulipia leseni za Biashara pamoja na hushuru wa huduma walipe bila kushurutishwa kwani muda uliwekwa na halmashauri hiyo umekwisha.

Aliwataka Wafanyabiashara wa Manispaa hiyo pamoja wenye viwanda kulipia kodi zao kwa Wakati ili kuondoa usumbufu.

Aidha JAMES alisema wiki hii yote manispaa ya Ilala itakuwa kazini huduma zitatolewa siku ya Jumamosi na Jumapili pia katika ofisi za halmashauri hiyo Arnatogluo Watumishi wote watakuwepo kwa ajili ya kurahishisha Jambo liende kwa wakati.

Alielezea kodi ya huduma alisema inalipwa na Wafanyabiashara wote kuanzia wadogo mradi uwe na leseni ya Biashara na kodi hiyo kwa mwaka ulipwa mara nne sio Manispaa Ilala peke yake ni MANISPAA zote kodi ipo kisheria.


Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: