Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kuwa hakuna mwanachama au kiongozi aliyehamia kwenye chama hicho kwa kushawishiwa na fedha.

Akizungumza kwenye mahojiano na TV E amesema kuwa wote wanahamia kwenye chama chao wamekuwa akieleza kuwa wamevutiwa kufanya hivyo.

"Hakuna hata Mwanachama au Kiongozi yoyote alienunuliwa kwa pesa kurudi ama kujiunga na
CCM. Wote wamekuwa na maelezo kwamba wamekuwa wanavutiwa na namna CCM na serikali zake na namna wanavyotekeleza ilani zake," amesema.
Dkt Bashiru Ally.

Hivi karibuni CCM walipokea ugeni mkubwa wa Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa aliyerejea kwenye chama hicho akitokea CHADEMA ambapo alitimukia huko mwaka 2015 na kupata nafasi kugombea urais.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: