Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aguswa na mama muuza vitumbua na kuamua kumuunga mkono ili kumuwezesha kuweza kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamejiri Leo Maeneo ya Muriet Mkoani Arusha baada ya Gambo kuzungumza na mfanyabiashara huyo na kumueleza changamato
anazokabiliana nazo katika biashara yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mhe. Gambo ameandika:
"Leo nipo Muriet nyumbani.
Nimepita kununua vitumbua vya
chai ya familia nyumbani.Mama huyu ameniambia yeye ana wateja wengi
tatizo mtaji wa kuanzia elfu 50.
Anasema akipata Lita 10 za mafuta na
kilo 10 ya unga wa ngano maisha yake yatabadilika.
Anasema alikuwa
anafanya kazi na kulipwa elfu 2000 kwa siku,kiasi hicho alipe
nauli,chakula na ahudumie familia.
Wakati wote amekuwa akienda na mtoto
mgongoni na kurudi saa 6 usiku nyumbani." Alisema Mhe Mrisho Gambo.
Hata hivyo Mhe.
Gambo ameahidi kumuunga mkono mfanyabiashara huyo mdogomdogo ili kuweza kufikia malengo yake.
"Nimeguswa na maelezo haya na nitamuunga mkono kwenye jitihada zake hizi za kujikomboa kimaisha".Alieleza Mhe.Gambo
Post A Comment: