NA
MWANDISHI WETU, SONGEA
MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi akiaambatana na Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika hilo wamefanya
ziara katika Mikoa ya Iringa Njombe pamoja na Ruvuma ili kujionea maendeleo ya
Miradi inayotekelezwa na Shirika katika Mikoa hiyo.
Katika
ziara hiyo Bodi ilitembelea vituo vya Gridi vya Makambako pamoja na Madaba
ambavyo vimejengwa kupitia Mradi wa ujenzi wa njia ya usafirishaji umeme wa
Kilovolti 220 wa Makambako -Songea. Pia Wajumbe walipata wasaa wa kutembelea
eneo la Kisada ambapo TANESCO inatarajia kujenga kituo kikubwa kabisa cha Kupoza
na kusafirisha umeme chenye uwezo wa kupokea umeme utakao safirishwa katika
njia ya umeme wa Kilovolti 400 ya Iringa hadi mbeya Njia ya usafirishaji umeme itakayo
ziunganisha nchi za Tanzania na Zambia. Hii ni miongoni mwa jitihada zinazo
fanywa na Serikali kupitia TANESCO za
kuunga njia za usafirishaji umeme za kusini mwa Bara la Afrika (South African
power pool)
Akizungumzia
umuhimu wa Miradi hii Dkt Kyaruzi alisema , inakusudia kuiunganisha nchi na
mataifa mengine yanayotuzunguka kwa upande wa Kaskazini ambako kuna mradi
ujulikanao kama Kenya-Tanzania Power
Interconnection (KTIPIP)ZTK na tayari umeanza kutekelezwa
(East African Power pool) pamoja na upande wa kusini katika( South African
Power Pool) hii itawezesha Tanzania kuweza kunufaika na umeme unaopatikana nchi
za Kenya na Ethiopia ambao tayari
watakuwa wamejiunga na mifumo yetu , vivyo hivyo kwa upande wa Zambia ambao pia
tutajiunga nao.
Pamoja
na kutembelea vituo hivyo wajumbe wa bodi walitembelea Kituo cha zamani cha
Kufua umeme kwa
kutumia mafuta ya Dizeli cha Songea
ambacho kimesitisha kutumika
tangu mwezi Septemba mwaka 2018 ili kupisha ujio wa umeme wa Gridi ya Taifa
kupitia Mradi wa njia ya Kusafirishaa
umeme ya Kilovolti 220 ya Makambako Songea. Ambapo kuzimwa kwa kituo
hicho kumeiwezesha TANESCO kuokoa zaidi
ya shilingi Milioni 430 kwa mwezi.
MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, (wapili kushoto-mbele), na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, wakitembezwa kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Songea, wakati bodi ilipotembelea miundombinu ya umeme
Mwendesha
mitambo "system operator " kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha
Songea, Bw. Athanas James Saga akitoa maelekezo ya usalama mbele ya wajumbe wa
bodi walipotembelea kituo hicho.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme(mstari wa mbele katikati) nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Post A Comment: