MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa kikao cha kuweka mikakati ya kukabiliana na biashara haramu za magendo wilayani humo kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally na Mkuu wa Bandari ya Tanga Percival Salama
 Mkuu wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Seif Ally
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa kikao hicho
 Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson George akizungumza wakati wa kikao hicho
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally akizungumza katika kikao hicho kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akiwa meza kuu na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Isaya Mbenje kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally
Afisa Tawala wilaya ya Pangani Gipson George kulia akiwa na wadau wengine wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
 Sehemu ya Watendaji wa Vijiji na Kata wilayani Pangani wakifuatilia kwa umakini hoja kwenye kikao hicho
 Sehemu ya watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa kwenye kikao hicho
 Sehemu ya watumishi wa Halmashauri wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
Sehemu ya vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Pangani wakiwa kwenye kikao hicho
MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah ametangaza vita mpya ya kupambana biashara haramu za magendo wilayani humo huku akieleza viongozi watakaohusika watawaondolewa kwenye nafasi yao na hata kama ikibainika yeye anahusika yupo tayari kuachia nafasi yake na kukaa pembeni.

Huku akieleza pia kwa yoyote ambaye atahusika kwenye biashara hizo za magendo ikiwemo viongozi wa vijiji, kata na madiwani watakaobainika kuhusika wataondolewa kwenye nafazi zao.

Vita hiyo aliitangaza jana wakati wa kikao cha pamoja baina yake na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani, wakiwemo madiwani, wenyeviti na watendaji wa Kata na Vjiji ikiwa ni sehemu ya  mkakati wa kupambana na biashara haramu za magendo wilayani humo.

Alisema haiwezekani viongozi wakawa wanashirikiana na wafanyabiashara kupitisha bidhaa za magendo na wao kuendelea kufumbia macho jambo ambalo linapelekea kuleta athari kubwa kwa uchumi wa wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla kutokana na kuendelea kufanyika vitendo hivyo .

“Labda niwaambia kwamba uwe Mwenyekiti wa Kijiji, Watendaji wa Vijiji na Kata wakiwemo Diwani ikibainika umehusika kupitisha bidhaa za magendo utupishe ukae pembeni na ukatafute kazi nyengine za kufanya “Alisema DC Zainabu.

“Lakini pia tuna taarifa kwamba wapo watu wanapokea mishahara miwili kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa kuhusu kuwapa taarifa za uwepo wa ulinzi ama la lakini niwaambie siku zao zinahesabika maana hawatapona kwenye vita hii “Alisema.

Alisema kwa upande wa watumishi wa serikali ambao watabainika kujihusisha na biashara za magendo nao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo

“Lakini niseme kwenye vita hii hatutakuwa na msalie mtume kwenye jambo hili hata kama ni mimi mnadhani najihusisha na biashara za magendo nitakaa pembeni.

Aidha alisema pia pamoja na kwamba vita hiyo ni ngumu lakini wataweka mikakati imara kuweza kukabiliana nayo kwa lengo la kuhakikisha inaondoka kwenye maeneo yao .

Aidha pia alisema ili kuhakikisha wanatokomeza vitendo hivyo huku wakiwatahadharisha wafanyabiashara watakaokutwa na bidhaa zisizokuwa na nembo ya Mamlaka ya Chakula na dawa nchini (TFDA) watakamatwa kutokana na kwamba vitakuwa bidhaa ambazo hazijalipiwa kodi.

“Lakini pia Nyumba ambayo itakutwa imehifadhi bidhaa za magendo atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma ambazo zinawakabili za kujihusisha mambo hayo “Alisema DC Zainabu.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Bandari ya Tanga Percival Salama alisema kitendo cha watu kupitisha mzigo kwenye bandaru bubu ni kuvunja sheria za nchi namba 17 ya 2004 na kifungu 47 ambacho kinaelekeza mizigo au abiria watashuka au kupakia eneo lilorasmi.

Alisema haitoshi watanzania wakawa watu wa pili kiichumi nyuma ya majirani zao kwani eneo linalotufanya kufika huko ni kukosa uadilifu na uzalendo wa kweli wa Taifa.

Hata hivyo alisema kila mtu lazima ajue ukiwa kiongozi kama ni sehemu ya rushwa unaua msingi wa kizazi chako mwenyewe kutokana na mambo utakayoyafanya hawawezi kwenda mbali.

Mwisho.


Share To:

Post A Comment: