Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu. Jerry Cornel Muro ameweka DHAMIRA yake ya kimkakati ya kubadilisha sekta ya KILIMO kutoka kilimo cha kutegea MSIMU na badala yake sasa Wilaya ya Arumeru itakuwa na kilimo cha moja kwa moja ambacho amekipa jina la OTESHA KISHA VUNA HALAFU OTESHA TENA .
Dc Muro katika kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa na unakiwa endelevu ameamua kuhusisha Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kuanzia Wakulima ,Taasisi na wizara za serikali zinazohusiana na Kilimo, Mbegu , Masoko pamoja na Taasisi za Fedha ambazo zitakuwa na wajibu wa kubadilisha mtazamo wa kilimo cha Arumeru .
Kwa kuanzia Dc Muro ameamua kuzishirikisha Taasisi za kitafiti za kilimo ambazo zitalazimika kufanya utafiti wa kina katika kufikia Azma hiyo, ikiwemo kushauri namna bora ya kutekeleza mkakati huo katika ngazi ya wilaya, ambapo amefanya ziara katika Taasisi ya Utafiti ya Mazao ya Kilimo Africa (IITA) Iliopo jijini Dar es salaam, na kukubaliana kuanzisha ushirikianona taasisi hiyo yenye ofisi zake Wilaya ya Arumeru.
Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara mbalimbali na kuzungumza na watumishi wa Taasisi hiyo DC Muro amesema dhumuni la kutembelea taasisi hiyo ni ili kujifunza na kujionea jinsi kazi zinavyofanywa katika Taasisi hiyo ya Kilimo.
"Leo nimejionea kazi inayofanywa hapa makao makuu lakini pia nimekuja kuweka mshikamano nakuongeza ushirikiano ambao unalenga pia kuwanufaisha wananchi wetu ambao ndio walengwa wakuu."Alisema Dc Jerry Muro.
Aidha DC wa Arumeru, Ndugu Jerry Muro* amemshukuru Rais Wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwakuanzisha kituo hicho kwaajili ya utafiti na maswala yote yanayohusu kilimo.
"Nianze Sana kwakumshukuru Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli lakini nimshukuru mtangulizi wake Rais Kikwete kwakuliona hili nakuona kuna uhitaji wa sisi Tanzania kuwa na senta hii kwa ajili ya utafiti na maswala yote yanayohusiana na kilimo". Alisema DC Muro.
Hata hivyo Dc Muro alisema kuwapo kwa taasisi hiyo kutasaidia kutoa fursa kwa wakulima nakuweza kupata elimu na mambo mbalimbali yanayohusuana na tafiti na ugunduzi katika sekta hiyo ya kilimo.
"Ujenzi wa Kituo hiki katika Nchi yetu ya Tanzania imetupa fursa sisi Kama watendaji wa Serikali kuweza kunufaika moja kwa moja na uwepo wa Taasisi hii Tanzania, Kwa mkoani Arusha ipo katika wilaya yetu ya Arumeru imesaidia pia kutoa fursa kwa wakulima wetu kuweza kupata kipaumbele katika Mambo mbalimbali yanayohusiana na tafiti na ugunduzi wa maswala mbalimbali katika sekta ya kilimo." Alieleza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu. Jerry Muro.
Awali akimkaribisha Dc Muro katika ofisi za Mkuu wa taasisi hiyo inayohudumia nchi za ukanda wa Africa Mashariki Dkt Victor Mayong mbali na kuipongeza serikali ya awamu ya tano katika kutengeneza mazingira bora yanayovutia uwekezajo kwenye Kilimo amesema wao wataendelea kushirikiana na serikali pamoja na nchi za Africa Mashariki katika kupambana na changamoto zenye viashiria vya kupunguza uzalisha wa chakula yakiwemo magonjwa kwenye mimea, na kusisitiza lengo la taasisi yao ni kubadili mfumo wa kilimo cha Africa na kuongeza uzalishaji wa mazao
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
27/03/2019
Post A Comment: