Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro akizungumza wakati wa halfa hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro katikati akiwa na wafugaji
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro akiwa amevaa nguo ya kimasai
 Sehemu ya mifugo wakinywa maji
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro kushoto akipata maelekezo
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro akitembelea maeneo mbalimbali
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro akizungumza jambo


Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Cornel Muro leo amekabidhi mabwawa manne makubwa yenye uwezo wa kuhifadhi na kuvuna maji ya Mvua Milioni Thelathini na nane za maji ya mvua ( 38,000,00 ) kwa Viongozi wa kata ya Oldonyosambu ambao wengi wao wanatoka katika maeneo ya Wafugaji kwa ajili ya matumizi yao na mifugo katika kijiji cha Lemanda.

DC Muro amekabidhi Mabwaya hayo , mara baada ya kuyapokea kutoka kwa wadau wa maendeleo Shirika la OIKOS la nchini Italia kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa ( EU ) Pamoja na ushirikiano wa nguvu za ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Arusha DC

Awali Mabwawa hayo yalikuwa na uwezo wa kukusanya na kuhifadhi maji lita milioni sita tu na sasa yamekarabatiwa na kutengenezwa kuweza kumudu kuhifadhi maji lita million 38, pamoja na ujenzi wa Mapalio ya kisasa ya kunyweshea maji mifugo inayotoka katika maeneo mbalimbali mkoani Arusha

*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru*
*10/03 /2019*
Share To:

Post A Comment: