Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa ushauri kwa baadhi ya wanafunzi
wa kike juu kujikinga na mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikiharibu ndoto
za wanafunzi wengi wa kike.
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akibadilisha mawazo na wanafunzi wa
kike wanaotoka kwenye shule za sekondari zaidi ya saba kwenye wilaya ya
Iringa pamoja na viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in
Africa
Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kutoka wa
mmoja ya viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in
Africa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa
kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye shule za
sekondari zaidi ya saba kwenye wilaya ya Iringa pamoja na viongozi wa
shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa wilaya ya Iringa
Richard Kasesela amewataka wanaume kulipa mshahara kila mwezi wake zao
endepo
watawakataza wake zao kufanyabiashara la sivyo wawaache wake hao
wafanyebiashara kwa uhuru.
Akizungumza na wanafunzi wa
kike wanaotoka kwenye shule zaidi ya saba za wilaya ya Iringa,Kasesela alisema hivyo kutokana na maswali
ya
wanafunzi hao waliouliza “kwanini wanaume wamekuwa wakiwakataza wake zao
kufanya biashara?”
Kasesela alisema kuwa wanawake
wamekuwa wafanyabiashara wazuri na wenye bahati ya kupata faida na kuweza
kuendesha family pamoja na kuongeza kipato cha familia,kumkata wanamke
kufanya
biashara kunadumisha uchumi wa familia na nchi kwa
ujumla.
“Naomba niwaambie wanafunzi
kuwa mama zenu ndio wamekuwa msingi mkubwa wa kuijenga familia na kuleta
maendeleo
ya familia pale panapokuwa na maendeleo baina ya baba na mama hapo ndio
familia
hizo utaona zinavyokuwa na maendeleo” alisema
Kasesela
Hata hivyo Kasesela
alisema,Wanawake wamekuwa waaminifu,watumiaji wazuri wa mikopo,wanajua
kupanga
bajeti za familia hivyo ukimwacha mwanamke afanye biashara kwa uhuru lazima
familia itapata faida kubwa tofauti na ukimyima mwanamke fursa ya kufanya
biashara.
“Wanaume ndio tumekuwa
tukilazimisha kuchukua pesa za mwanamke na kuzitumia vibaya na
kuwasababishia
hasara wanawake lakini ukiwaacha wafanye biashara utaona wanavyofanya
maendeleo
kwa kasi kubwa” alisema Kasesela
Kasesela aliwapongeza lyra in
Africa kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike juu ya kuvunja mila potofu za
kimila kwa wanawake ili kuwawezesha wanawake kushika nafasi mbalimbali ya
uongozi na kujikomboa kiuchumi.
“Lyra in Africa mmekuwa
mkiisaidia sana serikali ya wilaya ya Iringa kwa kuwajenga uwezo wanafunzi
wa
kike kwa kuwa kufanya hivyo kunasaidia kuikomboa jamii kwa ujumla hivyo
juhudi
zetu zinaonekana na mimi kama mkuu wa wilaya nafurahi uwepo wenu” alisema
Kasesela
Kasesela alisema,lyra in Africa
wamekuwa wakiboresha mazingira ya wanafunzi wa kike kwa kuwajengea mabweni
kwenye baadhi ya shule za sekondari zilizopo hapa katika wilaya ya Iringa
mkoani
Iringa hivyo ni lazima kuwapongeza kwa kazi kubwa
wanayoifanya.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
shirika la lyra in Africa mkoa wa Iringa Roserine Malike aliwataka
wanafunzi wa
kike kusimamia vilivyo ndoto zao katika maisha iliwayumbishwe na wanaume
yoyote
yule kwa lengo la kutengeneza maisha yao hapo
baadae.
“Nyie wanafunzi wa kike
mnatakiwa kuwa na msimamo katika maisha yenu kwa kipicho cha maisha ili
kujenga
maisha yaliyo bora na kuwa mfano kwa wanafunzi wengine wa kike kwa lengo la
kuikomboa wanafunzi wengine wa kike hapa nchini” alisema
Malike
Malike aliwataka wanafunzi hao
wakike kucha tabia ya kufanya ngono wakiwa bado wanafunzi na kuwasababisha
kuharibu ndoto zao wakiwa na umri mdogo na kuongeza kuwa na vijana wengi
mtaani
wasio na ajira.
“Nafikiri mmeona wasichana
wengi walipota mimba wakiwa mashuleni wanavyohangaika mtaani kwa kuwa
walipoteza ndoto zao wakiwa bado wadogo hivyo mnatakiwa kuwa makini na
kudanganywa na wanaume kwenye umri mlionao kwa kuwa starehi hizi zipo tu
kila
siku” alisema Malike
Nao baadhi ya wanafunzi hao wa
kike walimweleza mkuu wa wialaya changamoto ya mfumo wa elimu ulivyojikita
wanafunzi kutegemea kuajiliwa pindi wamalizapo chuo au elimu yote hivyo
wamemuomba kufikisha kilio hicho serikalini ili waangalie mfumo huo
upya.
Post A Comment: