Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah amekerwa na tabia ya wanasiasa kuingiza siasa kwenye miradi ya maendeleo huku wakijisifu kuifanikisha miradi hiyo badala ya kuishukuru Serekali iliyowaleta hao wahisani mpaka kufika ngazi ya chini na kuwapatia miradi ya maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa kwenye taki la maji lilopo katika kata ya Ifunda akiangalia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya kuwatua ndoo wanawake

Na Fredy Mgunda,Iringa
 
Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah amekerwa na tabia ya wanasiasa kuingiza siasa kwenye miradi ya maendeleo huku wakijisifu kuifanikisha miradi hiyo badala ya kuishukuru Serekali iliyowaleta hao wahisani mpaka kufika ngazi ya chini na kuwapatia miradi ya maendeleo.

Asia aliyasema hayo wakati wa kilele cha wiki ya maji yaliyofanyika kata ya Ifunda halmashauri ya Iringa Dc mkoani Iringa alipokuwa akimwakilisha
mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi aliyekuwa kwenye majukumu mengine na kuwataka
 
wanasiasa kuachana ma porojo za siasa kwenye maendeleo kwa kuwa miradi hiyo inawahudumia watu wote bila kuangalia itikadi ya vyama vya siasa.

Kuna watu wamekuwa wakileta siasa za ajabu kwenye maisha ya watu tumekuja kufungua miradi ya maendeleo anakuja mtu analeta siasa za maji taka kuwa watu wengine sijui hawajashiriki hapa tumekuja kufungua mradi wa maendeleo sasa hii kitu isijirudie kuanzia tena tukijakufanya maendeleo ya wananchi basi tufanye kazi za wananchi na tuachane na siasa muda wa siasa ukifika tutafanya siasa tena kwa uhuru bila kubuguziwa kwa sasa ni muda wa kazi”

Asia alisema kuwa maendeleo hayana itikadi za kisiasa na ndio maana Rais John Magufuli anafanya kazi usiku na mchana kwa ajiliya kuwatetea wanachi wanyonge bila ya kujali itikadi ya vyama vyao hivo ni vema kila mtu akatimiza wajibu wake kuwatumikia wanachi na kuachana
na siasa za ulaghai ambao haziwezi wasaidia kwaku watanzania wanajua nini kinachoendelea kwenye nchi yao.

Hata   Asia amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa mstari wambele katika kupigania na kulinda vyanzo vya majiili visiharibiwe ili viendelee kuwasaidia wao na vizazivijavyokwanimajiniuhai.

“Ndugu zangu serekali imefanya kazi kubwa sana kuwa tunawatumikia watanzania,Rais wetu mpenda amekuwa akiwatetea na kuwatumikia watanzania bila ya kujali jinsi rangi wala kabila hivyo tunapaswa kumuunga mkono kwani kazi anayo fanya ni kubwa mno na ndio maana leo munaona maendeleo makubwa sana hivyo ni vema hata hii miradi hii ya maji muitunze vizuri”
hata hivyo wananchi mkoani Iringa wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wametakiwa kuwa na utamaduni wa kupanda miti inayotunza vyanzo vya maji ili kuvitunza vyanzo hivyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema kuwa miti iliyopandwa kando kando mwa chanzo cha maji katika kata ya Ifunda inasababisha kukauka kwa vyanzo vingi vya maji.

“Jamani viongozi wenzangu ni lazima tutoe elimu kwa wananchi aina ya miti ya kupanda kwenye vyanzo vya maji au pembezoni ma mito yetu ili kulinda haya maji la sivyo tutajikuta tunapoteza vyanzo vyetu vya maji” alisema Abdallah

Kwa upande wake Injinia wa maji Adrew Kisaro kutoka halimashauriya Iringa vijijini alisena kuwa halimashauri hiyo imejipanga vema kumaliza tatizo la maji katika halmashauri hiyo ilikuwasaidia wananchi wao kuteseka na swala la maji kwa wananchi kote nchini.

“Mh leo ni wiki ya kufunga wiki ya maji halimashaurii yetu imejipanga vyema kukabilia na tatizo la maji na  leo tunazindua mradi mkubwa huu wa maji ambao wameufanya watu wa WARIDI chini ya serekali yetu hivyo
naamini tatizo la maji katika eneo hili”


Kasaro aliwataka wakazi wa maeneo hayo kutunza vyema mradi huo kwani umedharimu pesa nyingi ili uweze kuja kuwasaidia wao na vizazi vijavyo.
Share To:

Post A Comment: