Mtoa hudua katika wiki ya Maji Duniani toka Mamlaka ya majiSafi na MajiTaka (DAWASA) Tumaini Samwel akitoa elimu kwa mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimishpo ya wiki ya Maji Dunia iliyoanza leo Machi 16- 22, 2019 ambapo wananchi wanajitokeza kutoa matatizo yao pamoja na kupewa elimu juu ya matumizi sahihi ya maji na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Watoa huduma katika wiki ya maji Clementina Mbogellah (Kushoto) na Neema Mbalamwezi wakitoa elimu kwa mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam aliyejitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika kuadhimisha wiki ya Maji Dunia iliyoanza Machi 16- 22, 2019.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa DAWASA, Evelasting Lyaro akitoa elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji Duniani inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
Burudani za amsha amsha wiki ya maji Duniani zikiendelea katika mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.
 Afisa Mwasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi akitoa elimu na vipeperushi wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya maji Duniani inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka imeandaa utaratibu wa kusikiliza kero za maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Maji Dunia iliyoanza jijini Dar es Salaam. DAWASA wameandaa dawati maalumu pamoja na wataalam ambao watatatua kero za wateja wa Maji kuanzia Machi 16- 22, 2019. Lengo ni kuwezesha wananchi kupata majibu ya kina ya changamoto mbali mbali zinazohusu huduma za majisafi na majitaka. Kauli mbiu: 'Hakuna atakayeachwa: Kuongeza kazi ya upatinaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira kwa wote katika dunia inayobadilika kitabia nchi," -- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''
Share To:

Post A Comment: