Waziri
wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza
wakati wa kufungua bonanza la mpira wa miguu kwa watoto kike wa shule za
msingi, Sekondari na vyuo lililofanyika katika Wilaya Kasulu Mkoani
Kigoma huku likiwa limemebea ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni basi, Elimu
ni haki yangu. Kushoto ni Mwakilishi wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM)
Mariam Ntakisivya mwanzilishi wa bonanza hilo.
Mwakilishi
wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) na muandaaji wa Bonanza hilo Mariam
Ntakisivya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa bonanza la
mpira wa miguu kwa watoto kike wa shule za msingi, Sekondari na vyuo
lililofanyika katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma huku likiwa limemebea
ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni basi, Elimu ni haki yangu.
Waziri
wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipiga mpira
kuashiria ufunguzi rasmi wa bonanza la mpira wa miguu kwa watoto kike wa
shule za msingi, Sekondari na vyuo lililofanyika katika Wilaya Kasulu
Mkoani Kigoma huku likiwa limemebea ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni
basi, Elimu ni haki yangu.
Baadhi ya timu za watoto wa kike wa shule za msingi, Sekondari na vyuo wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho ya bonanza hilo.
Waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amefungua na
kushuhudia bonanza la mpira wa miguu kwa watoto kike wa shule za msingi,
Sekondari na vyuo lililofanyika katika Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma huku
likiwa limemebea ujumbe wa Mimba na ndoa utotoni basi, Elimu ni haki
yangu.
Akizungumza
katika bonanza hilo Prof. Ndalichako amesema kuwa masuala ya mimba na
ndoa utotoni zisiwe sababu za watoto kukatisha masomo yao, na ameitaka
jamii kuhakikisha tamaduni hizo zinakufa mara moja na kila mmoja awe na
wajibu wa kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza malengo yao kielimu.
Amesema
kuwa mpango wa Serikali kutoa elimu bure kwa wote umelenga watoto wote
wanufaike na mpango huo na kueleza kuwa Serikali haitawafumbia macho
wale wote wanaokatisha masomo kwa watoto wa kike kwa namna yoyote ile.
Katika
mashindano hayo zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washiriki zikiwemo
fedha taslimu pamoja na vyeti, washindi walioibuka katika bonanza hilo
ni pamoja na Chuo cha Ualimu Kabanga, chuo cha F.D.C, Kinkati sekondari
na chuo T.T.C Kasulu.
Pia
timu zote zilizoshiriki mashindano hayo zilipata jezi, mipira, vifaa ya
shule,taulo za kike huku wanafunzi wa chuo cha uwalimu Kasulu
wakiondoka na kombe baada ya kuongoza katika mashindano hayo,
wakifuatiwa na Murusi, Kinkati, Murubona sekondari, Muka sekondari,
Kasulu F.D.C, Bogwe Sekondari na Kabanga TC.
Bonanza
hilo liliandaliwa na mwakilishi wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM)
Mariam Ntakisivya na mashindano hayo kuitwa (Mariam Cup) kwa UWT Mkoa wa
Kigoma.
Post A Comment: