Kesho 30 October 2018 kutakuwa na Mchezo kati ya Yanga watakaokuwa wenyeji wa Lipuli Fc katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Kuelekea mchezo huo Yanga kupitia kwa mratibu wake Hafidh Saleh ametaja wachezaji ambao watakosekana kwenye mchezo huo dhidi ya Lipuli Fc.
Hafidh Saleh msomaji wa Kwataunit amewataja wachezaji hao kuwa ni Juma Mahadhi ambaye alifanyiwa Upasuaji, Papy Tshishimbi na Ibrahim Ajibu ambaye kwa siku ya jana alifika mazoezini lakini akashindwa kuendelea na mazoezi kutokana na maumivu.
Mratibu amefunguka kuwa baada ya hayo kutokea waliamua kumpumzisha Ajibu na tayari leo ataendelea na matibabu ili kuhakikisha anakuwa fiti.
Post A Comment: