Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia wanaume watano, kwa kosa la kujihusisha na kununua wanawake wanaofanya biashara ya ngono katika eneo la Uhindini jijini Dodoma.

Akiongea leo na wanahabari Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto, amethibitisha kuwa wanaume hao wamekamatwa kwenye oparesheni maalum ambapo jumla ya wanawake 22 wamenaswa.

''Tumekamata wanawake 22 maarufu 'changudoa' au 'dada poa' wanaojihusisha na biashara ya ngono na pia tumakamata wamiliki wa 'Bar' zinazohifadhi wadada hao lakini pia tumewakamata wanaume watano ambao wananunua wakinadada hao'', amesema Muroto.

Mbali na hilo Kamanda Muroto amebainisha kuwa asubuhi ya leo Oktoba, 9, 2018, wamemkamata mwanaume mmoja ambaye hajamtaja jina lake anayedaiwa kuingia jijini Dodoma leo asubuhi na kuanza kutapeli watu akijifanya ni askari wa usalama wa taifa.

Katika tukio lingine la tatu, Muroto amethibitisha kukamatwa kwa mwanaume mmoja ambaye alitoka jela kwa kumaliza kifungo chake, lakini baada ya kurudi uraiani ameanza kushiriki kwenye matukio ya uvunjani wa nyumba za watu na kuiba vitu mbalimbali zikiwemo Runinga na Kompyuta.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: