Na Mwamvua  Mwinyi,Babamoyo.

WAKAZI wa Kitame kata ya Makurunge wilaya ya Bagamoyo,Pwani wametoa kilio chao cha miaka mingi cha ubovu wa miundombinu ya barabara kutoka Gama-Kitame,yenye urefu wa km.9.5.

Ubovu wa barabara hiyo ,husababisha kutumia njia ya maji kwa kutumia majahazi nyakati za mvua njia ambayo ni ndefu na kuwapa tabu hasa wagonjwa watoto na akinamama wajawazito.

Akitoa kero hiyo katika ziara ya mbunge wa jimbo la Bagamoyo ,alhaj Dk.Shukuru Kawambwa aliyoifanya kata ya Makurunge ,mwenyekiti wa kitongoji cha Kitame ,Silvester Kangwe alisema ,
kukiwa na mvua barabara haipitiki kwakuwa huweka mfinyanzi.

Awali nao baadhi ya wakazi wa Kitame akiwemo Tobias Saidi na Lulu Seif walimuomba mbunge huyo ,kuwasaidia kufuatilia namna ya kujengwa kwa barabara hiyo .

"Kilio hiki ni cha kipindi kirefu ,tunaomba utumie nafasi yako kutusaidia ,tuweze kuondokana na changamoto hii, Tunahofia mvua zikianza kunyesha tena, mafuriko huzidi na kuharibu kabisa barabara hii " walisisitiza.

Akieleza ufuatiliaji wa suala hilo ,Dk.Kawambwa alisema kwa kushirikiana na mhandisi wa wilaya waliandika ombi kuangalia namna ya kujenga ujenzi wa uhakika wa kipande hicho cha barabara.

"Sasa barabara hizi zipo chini ya TARURA na fedha zilizotengwa kwa mwaka 2018/2019 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati ama matengenezo madogomadogo na sio ujenzi mkubwa "

"Habari hii sio nzuri kwenu ,"Kwa hesabu za harakaharaka inaweza kutumika zaidi ya sh.bilioni mbili ,fedha hiyo sio mchezo wa kitoto ,hivyo sitoweza kufanya danganya toto ,nitaendelea kufuatilia hadi hapo kero hii itakapopatiwa ufumbuzi";:alifafanua Dk.Kawambwa.

Akijibu suala la ukosefu wa nishati ya umeme, Dk.Kawambwa alieleza, kupitia REA ahadi aliyopatiwa kipindi cha nyuma imekwenda ndivyo sivyo ambapo kwasasa amepewa ahadi kwa baadhi ya vitongoji na vingine vimetolewa huku Kitame ikiwa haimo.
 Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Alhaj Shukuru Kawambwa akitolea ufafanuzi kero alizofikishiwa na wakazi wa Kitame wakati wa ziara yake aliyoianza ya kata kwa kata jimboni humo
 (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Wananchi wa jimbo la Bagamoyo, wakimsikiliza mbunge wao akitolea ufafanuzi kero alizofikishiwa na wakazi wa Kitame wakati wa ziara yake aliyoianza ya kata kwa kata jimboni humo (picha na Mwamvua Mwinyi)
Share To:

msumbanews

Post A Comment: