Vijana wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuonyesha uthubutu katika kujiajiri kwa kuzithamini kazi wazofanya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi na Ajira, Anthony Mavunde, wakati wa ufunguzi wa wiki ya vijana kitaifa inayofanyika katika viwanja vya Tangamano, Jijini Tanga.

Amesema vijana wanatakiwa kuzithamini shughuli wanazofanya kwa kuzipa kipaumbele ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na dhana ya kuajiriwa.

“Vijana muondokane na mawazo mgando kutegemea kuajiriwa badala yake wajikite katika kujiajiri na Serikali itawapa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuboresha mazingira ya shughuli mnazofanya,” amesema Mavunde.

Katika hatua nyingine  Waziri mavunde amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika sherehe za kilele cha mbio za mwenge zitakazofanyika Oktoba 14, katika viwanja vya Mkwakwani, mjini hapa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: