Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(katikati) akiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo jana jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi (wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu kero zao mbalimbali wazipatazo kuhusu eneo hilo la Mchinjio.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi(wadau) wa machinjio ya Vingunguti ambapo amewahakikishi serikali ya awamu ya tano ipo pamoja nao na amewaomba kulipa kodi ili kuinua uchumi wa Taifa.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega jana katika machinjio ya vingunguti jijini Dar es Salaam.
Wadau wa machinjio ya Vingunguti wakiendelea na kazi.(Picha na Emmanuel Massaka.)
SHILINGI bilioni tatu zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi unatarajia kuanza Novemba mwaka huu.
Uamuzi wa kutengwa kwa fedha hizo ni katika jitihada za kuondoa changamoto zinazoikabili machinjio hayo.
Hayo ameelezwa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega.
Ulega alifanya ziara fupi katika machinjio hiyo akiambata na viongozi wengine wa serikali wakiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Nyama, Dk wa Mifugo na Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na uzalishaji toka Wizarani.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega alielezwa changamoto zinazoikabili machinjio hiyo ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara wa nyama kutozwa ushuru mkubwa kwa mazao ya mifugo, ukosekanaji wa soko la uhakika la ngozi, ambapo Ulega amesema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ina mkakati kabambe wa kukabiliana na changamoto hizo.
Ulega amefafanua kwa kuanza na ujenzi wa machinjio mpya ya kisasa utakaofanyika kwa gharama hizo za fedha za Serikali.
“Wasimamizi wote wa ujenzi wa machinjio hii nawataka muhakikishe kuwa ujenzi huu unafanyika kwa haraka na ubora ili machinjio hii iweze kuchinja ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku kwa kuwa machinjio nyingi zilizojengwa hazijazingatia suala la uchinjaji wa kuku,” amesisitiza Ulega.
Post A Comment: