Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma kwa kipindi cha miaka saba kama ilivyokuwa awali.
Profesa Ndalichako aliyasema hayo mjini Pangani wakati wa Kongamano la Elimu wilayani Pangani lililoenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzoi shule ya sekondari Mwera mbapo alisema suala la muda wa elimu msingi lipo kwa mujibu wa sheria ya elimu ya mwaka 1982.
Alisema sheria hiyo imeweka bayana kwamba muda wa elimu ya msingi ni miaka saba na bado sheria hiyo haijafanyiwa marekebisho hivyo wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma miaka saba.
Akitolea ufafanuzi suala hilo alisema ikifika mahali kama kutakuwa na ulazima wa kubadilisha miaka ya kwenda shule kitakachotanguliwa ni kufanya marekebisho ya sheria kwa sababu jambo linalokuwa ndani ya sheria huwezi kulifanyia mabadiliko bila kuanza kufanya marekebishi ya sheria husika.
“Niwatoe hofu watanzania kwamba suala la kisheria huwezi kubadilika kwa tamko wala waraka wa kamishna wa elimu au kubadilika kwa maelekezo mengine yoyote bali linaweza kubadilika pale sheria ya elimu 1982 kwenye kipengine kinachoeleza muda wa elimu ya msingi miaka 7 kitakapofanyiwa marekebisho”Alisema Waziri Profesa Ndalichako
Alisema baada ya kufanyiwa marekebisho ndio inaweza kubadilika na haitakuwa kinyumenyume na itaweka bayana kwa sababu badiliko kama hilo ni kubwa la sera na kisheria hivyo watu watafahamu mapema.
“Kumekuwa na mchanganyika kwa sababu sera ya elimu ya mwaka 2014 imeonyesha serikali itakuja kuweka utaratibu lakini haikusema itaweka lini kwamba elimu ya msingi iwe lazima mpaka sekondari”Alisema.
Alisema bado hatujawa tayari kuwa elimu ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wote hivyo tunaendelea kuboresha elimu ya msingi na sekondari kuhakikisha mazingira mazuri ya kufundisha na walimu wa kutosha.
Alisema watakapoona wamefika mahali na kuona haja ya kufanya hayo watu wamekuwa wakiulizia serikali itawashirikisha wadau wote kwamba tunakwendaje huku akieleza mkakati ni serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia
Post A Comment: