Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula akiendelea na ziara ya Mtaa kwa Mtaa Kata ya Igoma Mitaa ya Kikwete, Igoma Magharibi, Igoma Mashariki pamoja na Mtaa wa Mkapa, amepata fursa ya kutembelea Kituo Cha Afya Cha Kata na kujionea ujenzi wa kituo cha Afya uvyoendelea unaosimamiwa wa wakandarasi Wazawa kwa utaratibu wa Force account. *Serikali imetoa shilingi 400,000,000.00 kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Igoma ndani ya miezi mitatu kwa kujenga majengo saba ikiwemo jengo la kuhifadhi mili ya marehemu, wodi ya watoto, Wanawake, Maabala, jengo la huduma za pamoja, mioonzi pamoja na chumba cha kusafishia nguo* Mhe Mabula amesema.

Mhe. Mabula akiwa mitaa hiyo amesikiliza kero za wananchi kupitia makundi mbali mbali kama Boda Boda, wachuuzi, wajasirimali wa Kahawa pamoja na kukamilisha ziara yake kwa kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara. Miongoni mwa maombi ya wananchi aliyoyapokea na kuhaidi kufanyia kazi kwa haraka ni pamoja na ombi la kuwa na kituo maalum cha Bus Makubwa Kata hiyo pamoja na ombi la wananchi kuwezeshwa mpango wa urasimishaji wa maeneo kwa upimaji shirikishi.

Mhe. Mbunge katika ziara hii ameambatana na Diwani, Diwani Viti Maalum Mhe Anifa Mhere, watendaji wa Kata na Mitaa, viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Igoma

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿








Share To:

msumbanews

Post A Comment: