Ratiba ya Kumuaga mtoto wa Mwalimu Mwakasege aliyefariki Alhamisi October 11 :- Mwalimu atawasili Dar leo Jumatatu, Jumanne mwili utaagwa Mbezi Beach Lutheran Church, Jumatano alfajiri ni safari kuelekea Mbeya, na Alhamisi ni mazishi Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya
Mahali ulipo msiba Msiba uko Dar kwa mdogo wake Mwalimu Mwakasege anaitwa Eng. Mwakasingila (Mzee wa kanisa wa KKKT Mbezi Beach) Jinsi ya kufika msibani Fika hadi Mbezi Beach Jogoo, unaingia barabara ya Karibu Art Gallery kuelekea TAG Mbezi beach kisha utaona vibao vinavyoelekeza msiba ulipo.
Ratiba ya Jumatatu Kutakuwa na sara ya pamoja na Mwalimu Mwakasege na familia yeke yote itakayofanyikia hapa msibani itakayoanza saa moja jioni, 7pm itakayoongozwa na Askofu , Mchungaji kiongozi na watumishi wengine Kuaga Mwili wa marehemu utaagwa Jumanne 16 Oct kanisani KKKT Mbezi Beach Dar, kuanzia saa nane mchana (2pm) Baada ya kuaga mwili utapelekwa airport kwa ajili ya maandalizi ya safari.
Kusafirisha: Mwili utasafirishwa Jumatano 17 Oct kwa ndege Mazishi: Yatafanyika alhamisi, Tukuyu, Mbeya 18 Oktoba,2018.
Muhtasari: Joshua amefariki ghafla baada ya kudondoka alhamisi tarehe 11 Oct 2018 akiwa kazini kwake World Bank Dar. Alikimbizwa Aga Khan hospital ila alifariki siku hiyo hiyo.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.
Post A Comment: