NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI Mkoani Tabora imemtaka mzabuni aliyeshinda na kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja kutoa huduma ya dawa na vifaa tiba (JAZIA- Prime Vendor System) kuhakikisha orodha ya dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba vilivyopo kwenye mkataba vinapatikana wakati wote ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba na Kampuni ya Chacha Magasi Pharmacy Ltd na Serengeti Care kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo ambazo hazipatikani Bohari Dawa(MSD).
Katibu Tawala Mkoa alisema afya bora ni kitu muhimu sana ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga fedha nyingi kwa ajili ya dawa na vifaa tiba ili kuwawezesha wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na kuongeza ndio maana hakuna sababu ya kutokuwepo dawa katika Kituo cha Afya chochote.
Aidha Makungu aliwataka Wakurugenzi Watendaji wote kuhakikisha wanasimamia makubaliano yaliyomo katika mkataba huo ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma kuagiza dawa kutoka Bohari ya Dawa(MSD) na zile zitakazokosekana MSD ziagizwe kwa Mzabuni aliyeingia na Mkoa huo Mkataba na siyo vinginvyo.
Alisema ni vema waka wanafuatilia ili kuhakikisha Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali wakati wote zinakuwa na dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba vya kutosha ili wagonjwa wasipate usumbufu.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema lengo la JAZIA ni kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba katika Vituo vya kutolea huduma, kuboresha uwazi na uwajibikaji kwenye matumizi fedha za umma na kupunguza muda wa kuomba na kupokea dawa na vifaa tiba.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maagizo kwa Mzabuni aliyeshinda kutoa huduma kupitia unajulikana kama Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kuzingatia maelekezo ya mkabata kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo mara baada ya kusaini mkataba huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Gunini Kamba akitoa maelezo mafupi kuhusu uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( mwenye suti ya bluu) akisaini Mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Sekiete Yahaya naye akisaini huku wakishuhudiwa na Mkurugenzi wa Chacha Magasi Pharmacy Ltd Chacha Magasi (wa pili kutoka kushoto) na Serengeti Care Albinus Mongore(kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Gunini Kamba(kulia aliyesimama)
Baadhi ya Watendaji kutoka Chacha Magasi Pharmacy Ltd na Serengeti Care wakifuatilia maelezo ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora kabla ya kusaini Mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo.
Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Tabora wakiwa katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( mwenye suti ya bluu waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa huo na watendaji wa Chacha Magasi Pharmacy Ltd na Serengeti Care mara baada ya kusaini Mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia ) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa (kushoto) wakibadilishana mawazo mara baada ya kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Peter Onesmo Maloda (kulia ) na Mwenyeikiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) Said Ntahondi (kushoto) wakibadilishana mawazo mara baada ya kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo
Post A Comment: