Rais Dkt. John Magufuli leo 19, Oktoba anatarajia kukutana na wachezaji wa timu ya taifa (Taifa Stars) Ikulu jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli pia anatarajia kula chakula cha mchana pamoja na wachezaji hao.
“Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Oktoba, 2018 atakutana na wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) na baadaye kula nao chakula cha mchana Ikulu Jijini Dar es Salaam.”, imesema taarifa hiyo ya Gerson Msigwa.
Taifa Stars ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wake wa nyumbani wikiendi iliyopita na kuibua matumaini ya nafasi yake ya kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika AFCON itakayofanyika mwakani nchini Cameroon.
Baada ya ushindi huo, Taifa Stars inakamata nafasi ya pili katika kundi lake la L ikiwa na alama 5. Uganda ikiongoza kundi hilo kwa alama zake 10, huku Cape Verde ikiwa na alama 4 na Lesotho ikiburuza mkia kwa alama zake mbili.
Post A Comment: