Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akizungumza wakati akifungua mkutano wa kikao kazi cha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa maafisa wa mikopo katika vyuo vikuu uliofanyika mjini Bagamoyo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul- Razq Badru.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB )Abdul- Razq Badru akitoa taarifa ya bodi hiyo katika mkutano wo katika bodi na maafisa wa mikopo katika vyuo vikuu nchini katika mkutano uliofanyika mjini Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adam Mwakalobo akizungumza kuhusiana na ofisi yake inavyoratibu masuala ya elimu ya juu nchini kwa kushirikiana na vyuo vikuu,katika mkutano wa maafisa wa mikopo vyuo vikuu ulifanyika mjini Bagamoyo.
Ofisa Mikopo wa Chuo cha Uhasibu Arusha Esther Mwigune akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasimi katika kikao cha HESLB na Maafisa Mikopo katika Mkutano uliofanyika Mjini Bagamoyo
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa mikopo wa vyuo vikuu.
MAOFISA wanaosimamia madawati ya mikopo vyuoni wametakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro ili kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora isiyokuwa na urasimu na badala yake wahakikishe wanaimarisha madawati hayo ili kuhakikisha wanafunzi wenye sifa na uhitaji wanufaika na mikopo kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe wakati akizungumza katika kikao kazi cha siku mbili cha maafisa hao kilichoanza mjini Bagamoyo.
Amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata Elimu ya juu bila kikwazo.
Profesa Mdoe amesema kwa mwaka wa fedha 2018/19 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 427. 5 ambapo jumla ya wanafunzi 124 watanufaika na mkopo huo, na kuwa ugawaji wa mikopo hiyo uzingatie haki, vigezo, kanuni na sheria.
“Nataka twende vizuri tukahakikishe huduma bora inatolewa katika mwaka huu mpya wa masomo ikiwa ni pamoja kutoa huduma bora,kusimamamia kumbukumbuku na kuhakikisha mawasiliano ya mara kwa mara yanakuwepo kati ya maafisa mikopo na bodi ya mikopo na kwa haipendezi maafisa mikopo kuwa chanzo cha migogoro,”amesisitiza Profesa Mdoe.
Profesa Mdoe pia ameitaka bodi hiyo kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utendaji kazi, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kuwasaka waajiri warejeshe fedha ambazo wafanyakazi wao walisoma kwa mkopo, ili fedha hizo zitumike kwa wanafunzi wengine.
Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul- Razq badru amesema kuwa maagizo yote yaliyolewa na Naibu katibu Mkuu watayasimamia katika utekelezaji wa ugawaji wa mikopo kwa wnanafunzi huku akikiri kuongezeka kwa idadi ya wanufaika wa mikopo hiyo inayotolewa na serikali.
“Bodi ya mikopo inaahidi kusimamia haki, vigezo, kanuni na sheria katika utoaji wa mikopo hiyo kwa wanafunzi kama ambavyo sheria zinavyoelekeza, niwasihi sana maafisa mikopo kufanya kazi kwa weledi na kuacha mazoea ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza,”alisisitiza Badru.
Post A Comment: