Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo kumuondoa mara moja Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Shinyanga Paschal Highmagway kwenye nafasi yake kwa kushindwa kusimamia Kazi za ujenzi lakini pia kumtetea Mkandarasi wa Afrique Enginearing and Construction company Ltd ili hali Mkandarasi huyo ameshindwa kukamilisha Kazi yake katika muda uliopangwa.
Waziri Ndalichako ametoa maagjzo hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa Miundombinu chuoni hapo unaotekelezwa na wakandarasi wawili tofauti ambapo Mkandarasi mmoja ni Masasi amekamisha Kazi yake kwa asilimia 98 huku Afrique company Ltd ikishindwa kukamilisha Kazi katika muda uliopangwa.
Kufuatia hali hiyo Waziri Ndalichako amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Diwani Athumani kuanza kuchunguza miradi inayotekelezwa katika chuo hicho pamoja na Maafisa manunuzi wa Wizara ya Elimu kwa kuwa katika Chuo hicho kuna dalili za rushwa.
Waziri pia amemwelekeza Mkandarasi Afrique Company Ltd kuhakikisha anafanya Kazi usiku na mchana ili kuhakikisha Kazi hiyo inakamilika ndani ya mwezi mmoja na kuwa tayar mkandarasi huyo ameshalipwa kiasi Cha bilioni 2 na milioni 700.
“Haipendezi viongozi wa umma kila siku kukemea watendaji, kutumbuana kila tunapokutana kwenye majukumu, tunatakiwa tunapokutana tuwe tunakaa na kufurahi lakini kwa mtindo huu wa kushindwa kukamilisha Kazi kwa wakati serikali haitamvumilia mtu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta mboneko amemhakikishia Waziri kuwa Uiongozi wa Wilaya utasimamia kwa karibu kuhakikisha maelekezo aliyoyatoa yanatekelezwa lakini pia amewataka wakandarasi wababaishaji wabadilike na wasipobadilika basi uongozi wa Wilaya utawabadilisha.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
5/10/2018
Post A Comment: