Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula amekabidhi vitabu 442 vya Sayansi, michepuo wa Art pamoja na uchumi katika shule ya sekondari Mahina iliyopo Kata ya Mahina. Vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi 12,000,000.00 ni msaada kutoka taasis ya SOS "Serve Our Soul" kwa dhima ya kuboresha sekta ya elimu Wilayani humu kwa kutekeleza kwa vitendo Sera ya elimu mwanafunzi mmoja kitabu kimoja. *Nina washukuru SOS kuwa wadau wa maendeleo Nyamagana, Shule ya Mahina mtumie msaada huu wa Vitabu kama ulivyokusudiwa, tuondokane na dhana ya kusifika kutokupenda kusoma* Mhe Mabula amesema
Akiongea kwa niaba ya uongozi wa Shule Mwalimu Mkuu Ndg. Samwel Makubi ameshukuru msaada huo utakao wezesha wanafunzi kujisomea na kuongeza maarifa sanjari na ufahuru. Mwl. Makubi amemuomba Mhe Mabula kuwasaidia kutatua changamoto ya matundu machache Choo ambapo kwa sasa yapo matundu sita kati ya wanafunzi 1140 ikiwa 521 wakiwa ni wanafunzi wakike.
Hafla hiyo imefanyika katika ziara maalum ya Mbunge Jimbo la Nyamagana katika taasis ya SOS akiambatana na viongozi wa SOS wakiongozwa na Kaimu Maneja Ndg. Samson, Mhe. Sima Constantine Dima, Uwakilishi wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata, watendaji wa Serikali Kata na mtaa pamoja na ujumbe wa Taasis ya First Community Organization.
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Post A Comment: