Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul ametangaza kujiuzulu wadhifa huo na kujiunga na CCM.
Barua inayosambaa kwa kasi mitandaoni kuanzia saa 4.20 usiku ikionyesha kwenda kwa Spika wa Bunge Job Ndugai ikiwa imesainiwa na Gekul anasema amejiuzulu uanachama na ubunge wake.
Ikiwa ni kweli Gekul kajiuzulu, atakuwa mbunge wa nane wa upinzani na tisa wa Bunge la 11 chini ya Spika Ndugai kujiuzulu.
Lazaro Nyalandu aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM alijiuzulu na kujiunga na Chadema.
Waliojiuzulu na kutimukia CCM walikopitishwa na kugombea na sasa ni wabunge ni; Maulid Mtulia (Kinondoni-CUF) na Dk Godwin Mollel (Siha-Chadema).
Wanaosubiri kuapishwa ni; Mwita Waitara (Ukonga-Chadema) na Julius Kalanga (Monduli-Chadema) huku Zuberi Kuchauka (Liwale-CUF) huenda akaibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika leo Jumamosi Oktoba 13,2018.
Wengine waliojizuli hivi karibuni ni; Mwarya Chacha (Serengeti-Chadema) na James Milly wa Simanjiro naye Chadema.
Post A Comment: