Na Shushu Joel,Dar
MIAKA 19 iliyopita taifa nilitapwa na msiba mkubwa ambao kamwe hautozibika katika taifa hilikwa kuodokewa na aliyekuwa mwasisi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyere ambae alipatwa na umauti huko nchini Uingereza.
Kwa wakati huo Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa alipoutangazia umma wa watanzania kuwa kipenzi,mzalendo,mpenda haki na kimbilio la wanyonge mwl Nyerere katutoka ,basi vilio toka mataifa mbalimbali vilisikika kwa kutambua thamani ya hayati baba wa taifa.
Akizungumza na vijana wasiopungua 300 katika ukumbi wa chuo cha usafirishaji (NIT) mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete amabye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka 19 ya mwl nyerere watu wengi wamekuwa wakiitumia siku hiyo vibaya kwa kukaa tu majumbani pasipo kuwa na misingi mizuri ya jinsi ya kuenzi kumbukumbuku hiyo ya baba wa taifa.
“Watanzania walio wengi wanatumia siku hii kwa kupumzika majumbani kwao tu,hivyo mimi kupitia vijana nimeamua kurudisha utamaduni wa kumuenzi mwl Nyerere kwa kutoa elimu kupitia mikutano yangu ya kibunge popote pale nitakapokuwa nazungumza lazima nitamtaja Hayati baba wa taifa”Alisema Kikwete.
“Kwa kuangalia picha,Video na kusikiliza vipindi vya Radio au sauti zake kupitia sehemu mbalimbali inawakumbusha watanzania wote kuwa ni nini hasa mwl Nyerere alikuwa akihimiza kuhusu maendeleo ya wananchi wake na hasa wakulima ambao wako wengi kuliko kwani ni asilimia 70 utegemea kilimo”
Alisema kuwa mwl alikuwa ni kiongozi wa kipekee kutokana na juhudi zake za kuhakikisha mtanzania yeyote yule ananufaika na raslimali zake na ndio maana alianzisha umoja mbalimbali kwa lengo la kuwataka watanzania wawe na umoja bila kuwepo kwa ubaguzi wa aina yeyote ile,akitolea mfano hivyo Kikwete alisema kuwa mwl alianzisha Azimio la Arusha ,Azimio la Musoma,Siasa ni kilimo,Uhuru na kazi hivi vyote vilikuwa na lengo la kuwataka watanzania wawe na umoja.
Aliongeza kuwa Hayati Baba wa taifa aliwataka watanzania kujishughulisha katika kilimo cha pamba,mkonge,chai,ufuta, korosho,mahindi na mazao mengine ya kibiashara kwa lengo la kujiajiri kupitia kilimo.
Pia Kikwete alisema kuwa mwl Nyerere alisisitiza uwepo wa viwanda vingi nchini utasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa vijana hivyo kila sehemu alihakikisha kuna viwanda kwa makusudi ya kuwasaidia vijana wa taifa hili,mbali na hilo mwl alikuwa mstali wa mbele katika kupinga rushwa kwa kusema kuwa rushwa nia adui mkubwa anayestahili kupigwa vita kila kona ya taifa hili.
Kupitia kongamano hilo Kikwete amemuomba Rais wa awamu ya tano Dkt Pombe Magufuli kuhakikisha juhudi zake za utitili wa viwanda na upingaji wa rushwa unafikiwa kwa asilimia kubwa ili kurejesha heshima iliyokuwepo miaka ya utawala wa hayati baba wa taifa.
Aliongeza kuwa serikali ya aamu ya tano kupitia Rais Pombe Magufuli na hasa yeye mwenye amekuwa kiongozi wa mstali wa mbele katika kumuenzi Hayati Baba wa taifa kwa vitendo kwa kufuata misingi mingi aliyokuwa akiifanya kipindi cha uhai wake,kwani Mwl Nyerere alisisitiza nchi ya viwanda kwa lengo la kutengeneza ajira kwa vijana,kuwafukuza kazi watumishi ambao sio waadilifu,kupiga rushwa na kuwathamini watanzania wanyonge kwa wakati wote.
Aidha alisema kuwa kupitia kongamano Kikwete aliongeza kuwa kupitia serikali ya awamu ya tano anahamini hakuna halmashauri nchini yenye viwanda vikubwa vilivyoanzishwa katika kipindi hiki na vimechangia kutokomeza tatizo la ajira kwenye jimbo lake ingawa bado wawekezaji wanazidi kumiminika kwa kuhitaji kujenga viwanda mbalimbali jimbo humo.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Ilala Sheila Lukuba amabye alimuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo amewataka vijana kutokubali kutumika vibaya na wanasiasa wenye nia mbaya na taifa letu kwani nchi inamalengo makubwa juu yao.
Aliongeza kuwa halmashauri ya Ilala imejipanga vizuri kwa kuhakikisha vijana wananufaika na taifa lao,ndio maana mpaka kipindi hiki Ilala inaendelea kutoa fedha kwa makundi tofauti tofauti kwa lengo la kuwakomboa na kuwafanya wawe wakuchangamkia fursa zinazopatikana hapa nchini.
Mbali na hilo katibu tawala huyo amempongeza mbunge Ridhiwani Kikwete kwa jinsi alivyomwelezeaHayati baba wa Taifa mwl Julius Nyerere kwa ufasaha mbele ya vijana wa jiji la Dar es Salaam,kwa elimu hiyo vijana watatambua umuhimu wa mwlimu Nyerere katika Taifa hili.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya changamka mwanamke Maria Lucas alimpongeza mbunge huyo wa chalinze kwa jinsi alivyowasaidia vijana hao kuweza kuelewa yale alikuwa akiyasisitiza mwl Nyerere enzi za uhai wake.
“Kama wakitokea viongozi wengine kama Ridhiwani Kikwete basi vijana wa leo tutanufaika kwa elimu ya kumtambua kwa ufasaha hayati mwl Nyerere ingawa tulio wengi atukumkuta ila kwa yaliyoelezwa na Ridhiwani ni kama tu nasi tumekuwa nae”Alisema
Aliongeza kuwa kutokana elimu ya kongamano ya kumjua mwl Nyerere nimegundua kumbe hakuna pengo katika nchi yetu kwani viongozi wengi wanafuata yale ambayo yalikuwa yakifanywa na mhasisi huyo wa taifa la Tanzania.
Pia amewataka vijana wengi hapa nchini kutumia muda wao kumsikiliza mwl Nyerere kwenye hotuba zake mbalimbali alizozitoa miaka ya nyuma ili kumuelewa zaidi kile alichokuwa akikihitaji kiwe katika nchi hii kwa makusudi ya kujenga uchumu wan chi na hata kuondokana na masuala ya kuomba omba katika mashirika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Mollel Foundation inayojishughulisha na kusaidia watoto njiti hapa nchini Bi, Dorice Mollel alisema kuwa vijana wanatakiwa kuwa wabunifu katika upazaji wa sauti kwani serikali ya awamu ya tano ipo kwa ajili yao,kumbukeni vijana wa leo ni viongozi wa kesho hivyo wanapaswa kutumiaujana wao vizuri katika kulisaidia taifa hili.
Naye Mratibu wa kongamano hilo Daudi Fadhili alisema kuwa wamefanya mpango wa kuwakutanisha vijana wengi zaidi ili waweze kumtambua mwl Nyerere kwa vitendo ili kuwasidia vijana hao kuweza kujua mambo mengi yaliyofanywa na mwl enzi za uhai wake.
Pia amempongeza mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete kwa kutambua umuhimu wa kuwapatia vijana elimu juu ya mwl Nyerere ili waweze kumtambua zaidi,akitolea mfano alisema kujwa mwl alikwisha wai kufukuza watumishi serikali kutokana na utendaji kazi mbovu uliogubikwa na rushwa ambapo Rais Magufuli anazidi kupambana nao.
Post A Comment: