Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Taifa (NEC) Dkt. Athumani Kihamia akiwa Liwale leo na kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi ndani ya jimbo hili. Picha na Vero Ignatus.
Mkurugenzi wa huduma za Kisheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi Emmanuel Kawishe.
Na. Vero Ignatus, Liwale,-Lindi
Maandalizi ya uchaguzi mdogo Jimbo Liwale Mkoani Lindi na kata nne Tanzania Bara yamekamikika kwa asilimia 100
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Taifa (NEC) Dkt. Athumani Kihamia kwamba vifaa vimefika wakati hivyo amewataka wananchi wa Liwale watambue kuwa uchaguzi siyo vita bali ni sera ya nchi ya kupata viongozi kwa kuchaguliwa,
"Vifaa vya uchaguzi vimefika kwa wakati, watendaji wa uchaguzi wamepatiwa mafunzo ya kutosha pia ulinzi na usalama umeimarishwa hivyo wananchi msiogope kuja kupiga kura hapo kesho".'' Kwa upande wa kampeni zipo salama hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kurupushani, hakuna malumbano yeyote makubwa ambayo yanaashiria ubunjifu wowote wa Amani''Amesema Kihamia.
Amesema vituo vya kupiga kura vitafunguliwa kesho saa moja asubuhi na vitafungwa majira ya saa kumi jioni 13oktoba 2018, hivyo wananchi wamejitokeze kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi ya Kikatiba ya kupiga kura.Aidha wananchi wametakiwa wakishapiga kura warudi manyumbani mwao na kuendelea na shughuli zao za kihalali zinazotekelezwa kila siku.
'' Hakuna haja ya kusema kuwa kuna mwananchi anayelinda kura maana tayari wana mawakala wao kayika mchakato mzima wa upigaji kura hadi kuhesabu hadi kumtangaza mshindi'',Mkurugenzi wa huduma za kisheria kutoka NEC Emmanuel Kawishe amesema hakuna changamoto ila baadhi vyama ambao hawakupata taarifa sahihi kuhusiana na maswala ya mawakala, hadi kufikia kusema tume imekataa wakati ilishakubaliana na vyama hivyo.
Ikumbukwe kuwa uchaguzi huo mdogo unafanyika katika jimbo la Liwale kutoka na aliyekuwa mbunge Zuberi Kuchauka wa awali kuhama kutoka chama cha CUF na kuhamia CCM.
Post A Comment: