Ndg. Salum Kalli Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana hivi Leo amekabidhi matofari 400 ya Saruji shule ya Msingi Bugando kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili, ikiwa ni msaada kutoka kwa Wanachama wa CCM shina la wakereketwa Magufuli Merelani  Soko Kuu Kata ya Pamba.

Akikabidhi msaada huu Ndg. Kalli amepongeza jitihada za Wafanyabiashara wadogo wadogo kwa jitihada za kuunga mkono serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais awamu ya tano Mhe. Dkt John Pombe Magufuli iliyoelekeza elimu bule kwanzia shule ya awali hadi sekondari.  *Matofari haya miliyoyatoa yanatoshereza ujenzi wa Vyumba vya madarasa viwili kwa kutambua chachu hii iliyoianzishwa na Shina la Wakereketwa wa CCM tawi la Magufuli Merelani nami natoa bando moja la Bati pamoja na kugharamia upakaji rangi wa Vyumba hivi* Amesema Ndg Kalli

Akimkaribisha Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Kalli, Diwani Viti Maalum Mhe. Sikitu Sanziyote amewapongeza sanaaa Shina la Wakereketwa Magufuli Merelani kushiriki shughuli za kijamii na  kuwahaidi ushirikiano wa dhati ili kuzidi kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.

Naye Mwenyekiti wa Shina la wakereketwa Magufuli Merelani Ndg. Bahati S Machemba amesema Shina hilo lilifunguliwa rasmi na Kaimu katibu wa Umoja wa Vijana Taifa Mhe. Shaka kwa lengo kuimarisha Chama Cha Mapinduzi baina yao, kuondoa dhana potofu kuwa, wafanya biashara wadogo wadogo wanapinga serikali iliyopo madarakani na kutumika kwa maslahi ya wapinzani. Ndg Machemba amesema kupitia shina hilo wameweza kukuza mitaji yao kupitia michango ya hiari sanjari na  kuunga mkono jitihada mbali za serikali ya CCM kwa shughuli za Jamii ikiwemo utoaji wa Matofari kwa shule ya msingi Bugando.

Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya uongozi wa shule ya Bugando Mkuu wa Shule Mwl. Fubusa Esrom amesema, msaada huo umekuja kwa wakati ikiwa shule imeanza ujenzi wa Vyumba vingine vya madarasa ilikusaidia wanafunzi kupata sehemu ya kusomea, sanjari kukabiliana na changamoto za uchakavu wa majengo, uhaba wa madarasa yaliyojengwa toka enzi za mkoloni mnamo mwaka 1938. Shule ya Msingi Bugando ina jumla ya wanafunzi 542 wakiwa wasichana 273, wavulana 227 na wanafunzi wenye mahitaji maalum  wakiwa 42.

Hafla hii imehudhuriwa na Mtendaji Kata ya Pamba Jonas Mgisha na watendaji wa serikali wa mitaa na Wenyeviti mitaa, viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya na Kata, na kushuhudiwa na wanafunzi pamoja na uongozi wa Shule mbili za Msingi Bugando pamoja na Miembeni.

Imetolewa na
Idara ya Siasa na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi
Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: