WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Serikali za Mitaa TAMISEMI Seleiman Jaffo,ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha anafanya ufuatiliaji wa masoko yote ya Wilaya hiyo ili kubaini changamoto zinazokabili masoko hayo.
Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipofanya Ziara katika Soko la Ferry Jijini Dar es Salaam na kufanya Tathimini ya maagizo aliyoyatoa katika soko Hilo miezi michache iliyopita.
"Kuna Migongano mikubwa Sana miongoni mwa wafanyabiashara,lakin Kuna Kodi nyingine zinatozwa kiholela Mkurugenzi fanya Ufuatiliaji huu"Amesema Waziri Jaffo.
Aidha amemtaka kufanya ufuatiliaji katika soko la Buguruni linalotegemewa kujengwa na kufahamu ujenzi unaanza lini na kukamilika kwa muda gani na kuongeza kuwa maeneo hayo wafanyabiashara wadogowadogo,wanashiriki kujenga uchumi wa Nchi kwa kulipa Kodi.
"Mkurugenzi mpya Hakikisha unatumia masoko haya kutengeneza ajira kwa Vijana,Hali kadhalika kupata Mapato ya Katika Manispaa yako ya Ilala"Amesema.
Waziri Jafo ameipongeza halimashauri hiyo,kwa kusimamia maagizo aliyoyatoa katika soko Hilo miezi michache iliyopita ambapo alitoa maagizo ya ukarabati wa barabara eneo la sheli na shimo lililokuwa katika soko Hilo kuzibwa ambapo yote yametekelezwa.
Pia waziri amemshukuru Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi kwa wafanyabiashara hao, sambamba na Mama Janeth Magufuli alietoa milioni 5 kwa ajili ya kina mama ntilie wa soko Hilo.
Post A Comment: