Oktoba 22, 1996, makamu mwenyekiti wa Chelsea, Mathew Harding alifariki dunia kwenye ajali ya helikopta, wakati akitoka kuangalia mechi ya Bolton Wanderers dhidi ya Chelsea.
Oktoba 27, 2018, mmiliki na mwenyekiti wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, amefariki dunia kwenye ajali ya helikopta, wakati akitoka kuangalia mechi ya Leicester City na West Ham.
Chelsea na Leicester City, zote hutumia rangi ya bluu na walipokezana ubingwa wa EPL, 2015, 2016 na 2017.
SRIVADDHANAPRABHA WA LEICESTER CITY.
Mwaka 2010, Vichai Srivaddhanaprabha aliinunua Leicester City ikiwa daraja la kwanza na kuwekeza pesa ya kutosha iliyoisaidia klabu hiyo kupanda ligi kuu 2014/15 na kutwaa ubingwa 2015/16.
Katika orodha wamiliki wa vilabu wenye mapenzi ya dhati navyo, Srivaddhanaprabha anakaa kwenye nafasi za juu kabisa akiwa na rekodi ya kuhudhuria asilimia kubwa sana ya mechi za Leicester City.
HARDING WA CHELSEA.
Mwaka 1993, mwenyekiti wa Chelsea, Ken Bates, alitoa wito kwa matajiri kuwekeza klabuni hapo ili kuokoa jahazi lilikuwa likielekea kuzama.
Harding, kama shabiki wa Chelsea tangu utotoni, akajitokeza na kuwekeza pauni ml. 26 zilizoiokoa The Blues na kuanza kujenga msingi mpya wa mafanikio ya sasa.
Kifo chake kilikuja miezi saba kabla ya Chelsea kutwaa taji kubwa la kwanza baada ya miaka 27, waliposhinda Kombe la FA.
Harding pia alitoa pesa zake kujenga moja ya majukwaa ya Stamford Bridge lenye uweso wa kuchukua watu 10,884. Kwa heshima yake, jukwaa hilo sasa linaitwa Mathew Harding Stand, kukiwa na kaulimbiu ya One Of Our Own
Post A Comment: