Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro wakati wa ufunguzi wa kikao cha ushauri  cha Wilaya hiyo  (DDC) ameeleza kuwa Wilaya hiyo  imejikita kwenye dira na mwelekeo wa Taifa hususani katika uchumi wa viwanda.
Mhe.Muro amefafanua kuwa  katika kuongeza kasi ya kuelekea uchumi wa viwanda Wilayani humo utatuzi wa changamoto mbalimbali ambazo ni vikwazo kwenye uwekezaji wa viwanda ikiwemo rasilimali ardhi  umepewa kipaumbele "ardhi ni rasilimali muhimu katika uchumi wa viwanda lazima tuwe na ardhi isiyo na migogoro ili kuvutia na kuimarisha uwekezaji wa viwanda katika wilaya yetu."amesema Mhe. Muro.
Aidha mwezi  Septemba mwaka huu, ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru iliendesha zoezi la utatuzi wa kero za wananchi lililokuwa na mafanikio makubwa kwani  mamia ya wananchi walipata utatuzi wa kero zao , zoezi hilo la utatuzi wa kero za Wananchi lililopewa jina la   "PAPO KWA PAPO"  lilifanyika kwa kuzingatia sheria ambapo  wanananchi waliokuwa na  kero mbalimbali walifika ofisi ya Mkuu wa wilaya na kusikilizwa  na jopo la wanasheria pamoja na wataalamu kutoka kitengo cha ardhi, ustawi wa jamii na Polisi hivyo wananchi walipewa ushauri wa kisheria pamoja na  msaada wa ngazi zinazofuata kwa utatuzi zaidi.
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka watumishi wa serikali kuanzia ngazi ya Vijiji wilayani humo kuwajibika ipasavyo kwa kuwa makini kwenye utendaji wao sambamba na kutoa huduma kwa wakati," msiwatese wananchi kutumia nauli na muda kuja kutoa kero katika ofisi yangu ambayo ingeweza kupata utatuzi katika ngazi ya kijiji,"Amesema Muro
Aidha Mhe.Muro amehitimisha mazungumzo yake kwa kuwakaribisha wadau wa kikao hicho kutoa ushauri na mawazo yatakayoweka mipango,  mikakati na maazimio yatakayo waletea wananchi wa Arumeru maendeleo na kudumisha Amani iliyopo.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro akizungumza  wakati wa ufunguzi wa kikao cha ushauri  cha Wilaya hiyo  (DDC)
Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Chembe akizungumza wakati wa kikao cha ushauri cha Wilaya hiyo( DDC).
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
Mwandisi wa Maji Halmashauri ya Meru Eng.Happness Mrisho akisoma taarifa ya idara maji ili wajumbe wa kikao cha DCC watoe ushauri utakao boresha sekta ya Maji.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Will Njau wakati wa kikao cha DCC.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Meru Mwl.Damari Mchome  akisoma taarifa ya idara ya Elimu Sekondari wakati wa kikao cha DCC.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Noah Lembris Saput wakati wa kikao cha DCC 
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru (kulia) na kaimu Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Arusha vijijini wakati wa kikao cha DCC.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Meru ,Wakili Magdalena John akitoa ushauri wa kisheria wakati wa kikao cha DCC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Will Njau akizungumza wakati wa kikao cha ushauri cha Wilaya ya Arumeru. 
Makatibu Tarafa wa Hlmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndg.Leonard Mpanju.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati wa kikao cha DDC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
Viongozi wa Vyama vya Siasa wakati wa kikao cha DDC.
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.


watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Arusha vijijini wakati wa kikao cha DDC.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: