Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro ameendelea kutatua kero ya Maji katika kata ya Tarakwa Halmashauri ya ARUSHA iliyo Wilaya ya Arumeru, Kwa kuweka Ubunifu wa kuunganisha wadau mbalimbali wa Maendeleo Wilayani Arumeru na kuwaomba kuungana nae katika kuleta Suluhu ya muda mfupi itakayosaidia kupatikana Kwa Maji wakati Serikali inaendelea na Mpango wa ujenzi wa Miundombinu itakayoleta Maji ya kudumu katika kata ya Tarakwa.

Dc Muro amewaeleza wadau hao kuwa wananchi wanachotaka ni Maji yawe yanakuja Kwa mpango wa muda mfupi au mrefu wao haiwahusu cha Msingi ni kuhakikisha Maji yanapatikana Kwa Njia yoyote ili kusaidia kina Mama na wasichana pamoja na Vijana wanaozunguka umbali mrefu kutafuta Maji badala ya kuendelea na shughuli za kuwaletea Maendeleo 

Dc Muro amefanikiwa kuwashawishi wadau na kumuunga mkono Kwa kutoa Malori yenye maboza ya Maji na kisha kuwayapeleka Kwa wananchi wenye uhitaji katika kata ya Tarakwa.

Nao baadhi ya Wananchi Waliokuwa na Uhitaji wa Haraka wa Maji wamepongeza ubunifu wa Mhe Dc Muro na kuweza kuwashawishi wadau kupeleka Maji katika kata yao ambapo wamesema kitendo kilichofanywa na Dc Muro ni Cha Kizalendo na kinapaswa kupongezwa na kila mwananchi wa Arumeru pasipo kujali Itikadi ya vyama vya kisiasa, dini au ukabila ambalo wamemtaka Dc Muro aendelee kuchapa kazi Kwa kuweka Misingi ya kizalendo.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru
Share To:

msumbanews

Post A Comment: