Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni za Hanspaul Group Satbir Hanspaul na Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za Hanspaul Kamaljit Hanspaul wakipokea tuzo kutoka kwa waandaji.


Usiku wa kuamkia leo Ijumaa October 26 2018 zimetolewa Tuzo maalum katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam Ambapo Kampuni Mama ya Hanspaul Group kutoka Arusha imeibuka moja ya washindi  Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampuni Mama ya Hanspaul Group Bwana Satbir Hanspaul amesema kwamba tuzo hizo ni heshima kwa watanzania wote, wafanyakazi na wateja wao.

Pia sambamba na hapo Mkurugenzi huyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk John Pombe Magufuli kwa kuweka mazingira bora ya ustawi wa viwanda hivyo kuweza kuifikia dhamira ya Tanzania ya Viwanda.

Ikumbukwe kuwa Kampuni za Hanspaul Group zimeendelea kutunukiwa tuzo hizo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa mwaka 2016-2017, 2017-2018 na 2018-2019.

Hanspaul Industries Limited inajihusisha na utengenezaji wa vifungashio vya bidhaa mbalimbali ilhali Kampuni dada ya Hanspaul Automechs Limited inajihusisha na utengenezaji wa bodi za magari ya utalii.


Baadhi ya picha mbalimbali kutoka kwenye tukio hilo.




Share To:

msumbanews

Post A Comment: