Mpaka usiku huu jumla ya watu 44 wanaripotiwa kufariki dunia na wengine 37 kuokolewa baada ya Kivuko cha MV Nyerere mkoani Mwanza kinachofanya safari kati Bugorora katika Kisiwa cha Ukerewe na Kisiwa cha Ukara katika Ziwa Victoria kuzama leo Alhamis Septemba 20,2018 mchana katika ziwa Victoria.
Kwa Mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella zoezi Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere limesitishwa kutokana na giza, na litaendelea kesho alfajiri.ambapo hadi sasa waliyookolewa wakiwa hai ni 37, waliokufa 44.
#UPDATES:Zoezi la uokoaji wa abiria waliokuwemo katika kivuko cha MV Nyerere limesitishwa kutokana na giza, na litaendelea kesho alfajiri.ambapo hadi sasa waliyookolewa wakiwa hai ni 37, waliokufa 44.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara.
Kamanda Shana amesema kuwa kivuko hicho kimezama leo mchana baada ya kupinduka. “Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka,” amesema.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho Kivuko hicho cha Mv Nyerere kina uwezo wa kubeba abiria 100, tani 25 za mizigo na magari madogo matatu.
Post A Comment: