Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi aakifafanua jambo awakati akizungumza na Wamachinga wa Mkoa wa Iringa, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya makundi mbalimbali ya jamii mkoani humo.Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara hao maarufu Machinga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameeleza mikakati ya serikali ya mkoa ya kuwatetea na kusimamia maslahi ya wamachinga ili watambuliwe na kusaidiwa kufanya shughuli zao vizuri.
Baadhii ya Wafanyabiashara hao a.k.a Wamachinga wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Ally Hapi alipokutana nao na kuzungumza nao mambo mbalimbali.
Awaahidi kuwa serikali itaendelea kuwa mtetezi wao siku zote
Wampa tuzo ya Rais Magufuli kwa utekelezaji wa ilani, kuwatetea
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amekutana na kuzungumza na wamachinga wa Mkoa wa Iringa ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya makundi mbalimbali ya jamii mkoani humo.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wafanyabiashara hao maarufu Machinga, Mkuu wa Mkoa wa Iringa ameeleza mikakati ya serikali ya mkoa ya kuwatetea na kusimamia maslahi ya wamachinga ili watambuliwe na kusaidiwa kufanya shughuli zao vizuri.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watendaji wote wa Mkoa wa Iringa kutowahangaisha machinga na badala yake kuwatengea maeneo mazuri ya biashara, kuanzisha magulio, kuwapanga vema machinga na kuwawekea utaratibu mzuri wa kuchangia maendeleo ya nchi yao jambo ambalo machinga wameeleza kuwa tayari kulifanya.
Aidha Hapi ameeleza kutoridhishwa na manispaa ya Iringa kushindwa kukusanya mapato kikamilifu kutoka kwa machinga wote ambao wamekuwa na utayari wa kuchangia mapato.Kati ya machinga zaidi ya 2000 waliopo, taarifa za manispaa ya Iringa zinaonesha ushuru unakusanywa kwa machinga 353 pekee.Mkuu wa Mkoa ameagiza jambo hilo kurekebishwa haraka.
Katika hatua nyingine, uongozi wa Machinga umemkabidhi RC Hapi hati maalum ya shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kwa jinsi serikali yake ilivyokuwa mtetezi wa wamachinga wakati wote.
Mikutano hii ni utangulizi wa ziara kubwa ya Mkuu wa Mkoa ijulikanayo kama IRINGA MPYA tarafa kwa tarafa inayotarajiwa kuanza tarehe 8 septemba wilayani Mufindi na kisha wilaya za Kilolo na Iringa.
Post A Comment: