Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani unaanza leo tarehe 06 Septemba, 2018. Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani Athumani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
Kamishna Diwani Athumani anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Post A Comment: