Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Steven Wasira kuwa mwenyekiti wa bodi ya chuo cha mwalimu Nyerere nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mark Mwandosya.

Aidha, wakati huo huo Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Festus Bulugu kuwa mwenyekiti wa baraza la uwekezaji la wananchi kiuchumi.

Dkt. Limbu anachukua nafasi ya Dkt. John Jungu ambaye amekuwa Katibu Mkuu wizara ya Afya, Jinsia Wazee na Watoto.

Itakumbukwa Dkt. Festus Burugu Limbu alikuwa mbunge wa Jimbo la Magu mkoani Mwanza, kwa awamu tatu tofauti akianza mwaka 2000 hadi 2015 na Stephen Masato Wasira alihudumu kama Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini kutoka mwaka 2005 hadi 2015 ambapo aliangushwa na Mbunge wa sasa Easter Bulaya.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: