Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Bunda mjini wakati akiwa njiani kuelekea Musoma mkoani Mara.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Bunda wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama kuwasalimia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi kwa njia ya Simu kuhusu mgogoro wa ardhi uliopelekea Bibi Nyasasi Masige mwenye kilemba aliyekaa kudai kunyang’anywa Kiwanja chake Wilayani Bunda. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Bibi Nyasasi Masige kiasi cha Shilingi laki tano ili zimsaidie mara baada ya kusikiliza kero yake ya madai ya kunyanga’nywa kiwanja chake. Rais Dkt. Magufuli ameagiza uchunguzi ufanyike haraka ili haki ya bibi huyo iweze kupatikana. PICHA NA IKULU
Share To:

msumbanews

Post A Comment: