Vijana mkoani Mwanza wamelishukuru Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuwa karibu na vijana wanaopata huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo.

Wakizungumza jana Septemba 8,2018 wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika katika Viwanja vya Lessa Garden Hotel jijini Mwanza,vijana hao walisema shirika la AGPAHI limekuwa msaada mkubwa kwa vijana kwani mbali na kutoa huduma kwenye vituo vya tiba na matunzo pia limekuwa likiandaa michezo kwa vijana.

Aidha walisema lengo la bonanza hilo lililokutanisha vijana wanaotoka katika klabu za vijana zilizoundwa na zinasimamiwa na AGPAHI katika halmashauri mbalimbali ni kwa ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na kujifunza.

Akifungua bonanza hilo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza aliwataka vijana kutokata tamaa katika maisha huku akiwasititiza kuwa wamoja na kuendelea kushirikiana.

“Nawaomba vijana ambao wamepata maambukizi ya VVU kuendelea kuwa wafuasi wazuri wa dawa za kufubaza makali ya VVU ARVs,kwani kupata maambukizi haimaanishi ndiyo mwisho wa maisha”,alisema Mbwiliza.

Naye Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona alisema vijana walioshiriki katika bonanza ambalo limefadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC) wanatoka katika halmashauri za wilaya za Misungwi,Sengerema,Nyamagana,Magu na Kwimba.

Alitumia fursa hiyo kuwasihi vijana kutafakari kwa makini kabla ya kufanya maamuzi katika maisha na kuepuka kupoteza mwelekeo kutokana na maneno ya watu wanaowazunguka katika jamii.

Miongoni mwa michezo iliyofanyika katika bonanza ni kukimbia mita 100,mbio za magunia,kushindana kunywa soda,mchezo wa chupa,kukimbia na malimao na mayai,kabute,kuruka ndoo,kukamata limao kwenye maji kwa meno,maigizo na vichekesho.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI WAKATI WA BONANZA LA MICHEZO
Katikati ni Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza akifungua bonanza la michezo kwa vijana kutoka halmashauri za wilaya mkoani Mwanza. Kushoto ni Mratibu wa Wahudumu wa jamii (HBC) kutoka halmashauri ya wilaya ya Misungwi Yahaya Isangula,kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza akiwasisitiza vijana kutokata tamaa katika maisha.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akielezea lengo la bonanza la michezo.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akiwataka vijana kushiriki ipasavyo katika michezo iliyokuwa imeandaliwa.
Vijana wakiwa katika viwanja vya Lessa Garden Hotel wakijiandaa kuanza kufanya michezo mbalimbali.
Katikati ni Mwenyekiti wa Kikundi cha vijana cha 'Wise Youth' kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, Douglas Renatus akitoa mwongozo wa kufanya michezo kwenye kundi lake wakati wa bonanza.
Kiongozi wa Kikundi cha vijana cha 'Wise Youth' kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando,Joan John akiongoza mchezo wa kabute.
Mchezo wa Chupa ukiendelea: Washiriki wa mchezo wakikimbizana na atakayewahi kukamata chupa ndiyo mshindi.
Mchezo wa kukamata limao kwa meno ndani ya ndoo ya maji kisha kushika chupa iliyopo katikati ukiendelea.
Mshindi wa mchezo wa kukamata limao kwa meno ndani ya maji akiwa na limao lake na chupa.
Mchezo wa kuruka ndoo: Kijana kafunikwa uso kisha kaambiwa kuwa kuna ndoo ya maji airuke.
Kijana akiruka juu akiamini kuwa kuna ndoo ya maji mbele yake.
Vijana wakiwa katika duara wakicheza mchezo wa kabute.
Mbio za magunia nazo zilikuwepo.
Mchezo wa kukimbia na mayai kwenye kijiko mdomoni ukachukua nafasi.
Mbio za kukimbia na malimao nazo zilikuwepo.
Mbio za mita 100 zikiendelea.
Vijana wakishindana kunywa soda haraka.
Vijana kutoka halmashauri ya wilaya ya Sengerema wakionesha mchezo wa Vichekesho.
Vijana wakionesha igizo kuhusu umuhimu wa wana ndoa kupima VVU.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia michezo ya vijana.
Kijana akiimba shairi.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akiongoza kipindi cha maswali na majibu wakati wa bonanza hilo.
Kijana akielezea mambo mbalimbali aliyojifunza wakati wa bonanza hilo.
Katikati ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akitoa mwongozo wa kugawa zawadi kwa washiriki wote wa bonanza hilo.Kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Leah Kisamo. Kushoto ni Mratibu wa Wahudumu wa jamii (HBC) kutoka halmashauri ya wilaya ya Misungwi Yahaya Isangula.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akionesha zawadi ya chupa kwa ajili ya washiriki wa bonanza la michezo.
Meza kuu wakijiandaa kukabidhi zawadi kwa washiriki wa bonanza hilo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza akikabidhi zawadi ya chupa ya maji kwa vijana.
Zoezi la kugawa zawadi ya chupa za maji likiendelea.
Pudensiana Mbwiliza akiendelea kugawa zawadi kwa vijana.
Walezi wa vijana nao walipata zawadi ya chupa za maji.
Wa pili kushoto ni Mwandishi wa Radio Free Africa Debora Mpagama akishikana mkono na Mwenyekiti wa Kikundi cha vijana cha 'Wise Youth' kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mike Kennedy baada ya kumpa zawadi ya chupa ya maji.
Picha ya pamoja washiriki wa bonanza la michezo.
Picha ya pamoja washiriki wa bonanza.
Picha za vurugu washiriki wa bonanza la michezo.
Picha ya pamoja Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania, Pudensiana Mbwiliza na walezi wa vijana mkoani Mwanza.
Kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akimpa zawadi ya maua Pudensiana Mbwiliza ikiwa ni sehemu ya pongezi kwake kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Vijana Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi Tanzania hivi karibuni.
Cecilia na Douglas wakimpa zawadi ya maua Pudensiana.
Pundensiana akiwa na maua yake.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share To:

Anonymous

Post A Comment: