Wananchi na viongozi wa wilaya ya Nzega wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuifanyia ukarabati mkubwa wa hospitali ya wilaya ya Nzega.
Shukrani hizo zimetolewa wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea wilayani hapo kuangalia maandalizi ya ukarabati wa hospitali hiyo ya wilaya.
Hospitali hiyo imepokea sh. milioni 800 ili kujenga majengo kwa ajili ya huduma zote za uzazi pamoja na ukarabati na ujenzi wa wodi ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Katika Ziara hiyo Waziri Jafo amezielekeza Halmashauri ya wilaya ya Nzega na ya Mji Nzega kuunda timu ya pamoja ya usimamizi wa ujenzi huo ili mradi huo ukamilike ndani ya miezi mitano.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua maeneo ambapo majengo mapya yatajengwa katika hospitali ya wilaya ya Nzega.
Viongozi wa Nzega wakimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo.
Wananchi wa Nzega wakisubiri huduma katika hospitali ya wilaya ya Nzega.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akitembelea kukagua miundombinu ya hospitali ya wilaya ya Nzega
Post A Comment: